• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. SAMIA ASEMA UMEME WA KUTOSHA UMEPELEKWA VIJIJINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 26, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA ASEMA UMEME WA KUTOSHA UMEPELEKWA VIJIJINI

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na   MUSSA YUSUPH,

LINDI 


MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imepeleka umeme wa kutosha vijijini ambao utaweza kuhudumia kongani za viwanda.

Dk. Samia aliyasema hayo alipohutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Alisema serikali imetanguliza nishati ya umeme ya kutosha kwa lengo la kuanzisha kongani za viwanda kwa sababu sekta ya hiyo inakuwa kwa kasi.

Dk. Samia alibainisha kuwa umeme huo utarahisisha maendeleo ya viwanda na kukuza uzalishaji.

Katika mkutano huo, Dk. Samia alieleza mkakati wa kudhibiti wanyamapori waharibifu wanaovamia mashamba ya wananchi.

Dk. Samia alisema serikali inafahamu mahitaji ya wananchi yanaongezeka, kwa sababu hiyo itaendelea kufanyia kazi sekta zote za maendeleo ya jamii ili wilaya hiyo ipige hatua zaidi.

“Vituo vya afya nane vipya vimejengwa, nikawa namuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) mnakata ngapi? Akaniambia zipo kata zaidi ya 20, nikaelewa kwamba kazi bado ipo.

“Bado tutakuja kujenga vituo vya afya, bado tutakuja kujenga zahanati, shule za msingi na sekondari. Tutahakikisha miradi yote ya maji inayotekelezwa inakamilika ili kila Mwanaruangwa apate maji safi na salama,” alibainisha.

Vilevile, alisema serikali inakwenda kukamilisha kuunganisha umeme katika vitongoji kuwezesha nishati hiyo ikatumike nyumbani, kulinda usalama na shughuli za uzalishaji.

“Niwaahidi kwamba kazi ipo na tunakuja kuifanya. Naelewa katika maeneo ya vijiji vya Madangilo, Magawa, Lugombe na Mbwemkulu kuna tatizo la wanyama kufanya uharibifu kwenye mashamba.

Alibainisha: “Hili ninalielewa vyema na mkiwakuta wale wanyama waambieni dawa yao ipo jikoni. Wanyama tunawapenda lakini lazima tuwalinde, tuwazuie wabaki kwenye hifadhi zao.”

Alisema hatua mbalimbali zinachukuliwa kuhakikisha wanyamapori hawaingii katika mashamba ya wananchi.

Previous Post

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

Next Post

CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

Next Post
CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAGOLI AFUNGUKA SIMBASC

MAGOLI AFUNGUKA SIMBASC

4 months ago
RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?