• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 20, 2025
in Habari, Siasa
0
NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na REHEMA MAIGALA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema ataongoza wizara hiyo kwa kuzingatia ushirikiano, kuheshimu mfumo wa utawala na kuhakikisha miradi na mipango iliyoanzishwa inaendelezwa bila kupoteza rasilimali.

Akizungumza katika makabidhiano ya ofisi hiyo jijini Dodoma, Simbachawene alisema bado ana moyo wa kujitolea na kutumia uzoefu alionao, kujazia mapengo yaliyopo hasa maeneo ambayo aliyawahi kuanzisha kwa misingi thabiti, alipokuwa waziri wa wizara hiyo.

Alisema inasikitisha kuona baadhi ya mambo mazuri yaliyoanzishwa kwa kutumia rasilimali za serikali, yakisimama baada ya wahusika kubadilika.

Alisisitiza kuwa, rasilimali yakiwemo mawazo yaliyowekwa katika maandishi, havipaswi kupotea, hivyo atahakikisha anazitafuta taarifa zote muhimu  kuendeleza kazi.

Simbachawene, alisema alikuwa akiandika kwa umakini wakati akikabidhiwa na mtangulizi wake, Innocent Bashungwa, kwa sababu, anatamani kuendelea kujifunza, akibainisha hakuna mtu mwenye haki miliki ya uelewa.

Pia, alisema katika utumishi wa umma, watu husaidiana kufanikisha majukumu, anaamini hata yeye, ataendelea kupata maarifa mapya kila siku, licha ya kuonekana ana uzoefu mkubwa.

Simbachawene aliongeza kuwa yeye ni muumini wa mgawanyo wa majukumu kama ulivyoelezwa katika miundo ya kazi za serikal.

Waziri Simbachawene, alimhakikishia Bashungwa kuwa, atasimamia utendaji kwa kuzingatia utaratibu na nguvu ya mfumo wenyewe.

Pia, alimpongeza Bashungwa kwa kazi kubwa aliyofanya, akisema amefurahishwa na namna alivyoweka mambo katika mpangilio.

Aliahidi kuhakikisha hakuna kazi inayoanza upya bila sababu, bali ataendeleza hatua zilizofikiwa kutimiza malengo.

Kwa upande wake, Bashungwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, alisema yuko tayari kushirikiana na Simbachawene wakati wowote akihitajika.

Previous Post

CCM: TUTAISIMAMIA SERIKALI

Next Post

RAIS DK. MWINYI AITA WAWEKEZAJI Z’BAR

Next Post
RAIS DK. MWINYI AITA WAWEKEZAJI Z’BAR

RAIS DK. MWINYI AITA WAWEKEZAJI Z'BAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI

MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI

2 months ago
LIVERPOOL, ARSENAL KAZI IPO

LIVERPOOL, ARSENAL KAZI IPO

8 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?