• ePaper
Friday, May 1, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUTAILINDA NCHI YETU KWA GHARAMA – PM MWIGULU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 26, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
TUTAILINDA NCHI YETU KWA GHARAMA – PM MWIGULU

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania, kuwa makini dhidi ya makundi ya watu wenye nia ovu ya kuichafua na kuiharibu Tanzania kwa maslahi binafsi.

Dk. Mwigulu, amesema serikali itawalinda Watanzania na rasilimali zake zote kwa gharama yoyote kupitia vyombo vya ulinzi na usalama.

Waziri Mkuu, aliyasema hayo kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani, yaliyofanyika katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na wahariri wa vyombo vya habari, Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu, alisema Tanzania ni nchi nzuri, hivyo Watanzania wanapaswa kuwa makini dhidi ya watu wenye nia mbaya.

Alisema wasioitakia mema Tanzania, wanatamani mabaya zaidi yaendelee kutokea, kwa hiyo, aliwasihi wawakatae na wasitumiwe kufanya uovu dhidi ya nchi yao.

“Kila mmoja alibebe jambo hili kwa ukubwa, hawatupendi, wanaangalia rasilimali zetu, nchi yetu siyo masikini, kuna watu wanamezea mate rasilimali zetu, ninawahakikishia kuwa tutailinda Tanzania na rasilimali zake kwa gharama yoyote.

“Kila Mtanzania anapaswa kuwa na dhamira ya dhati na kuunganisha nguvu katika kulinda na kuitunza Tanzania, tumtangulize Mungu na tuilinde Tanzania, viongozi wa Serikali katika ngazi zote, hakikisheni mnakuwa makini na kila anayeingia katika maeneo yenu.

“Tanzania haitaendeshwa kwa rimoti, Tanzania ni ya Watanzania na rasilimali zake ni za Watanzania. 

“Tutalinda Tanzania na rasilimali zake wala hatuna rekodi ya kushindwa. Hatujawahi kuwa na rekodi ya kushindwa,” alisema.

Alisema kuchoma ofisi za serikali 756, vituo vya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) 27, huku ikifahamika maisha ya Mtanzania Dar es Salaam ni kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Alisema hakuna Mtanzania ambaye amejilimbikizia mali kwamba, anaweza kukaa ndani mwaka mzima pasipo kutoka kujitafutia.

“Kuharibu mabasi sita, nyumba binafsi 273, vituo vya polisi 159, vituo binafsi vya mafuta 672, haya mafuta si ya mwenye kituo, magari ya watu binafsi 1,642, pikipiki binafsi 2,268, magari ya serikali 976 na hizi ni takwimu za mwanzo.

“Miaka yote hawajatokea wanaoipenda Tanzania, hii inakuja baada ya mradi mkubwa wa LNG ambao utafanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa gesi asilia duniani au wakati huu, ambao Tanzania itakuwa moja ya nchi tano mzalishaji mkubwa wa makaa ya mawe na kipindi ambacho yamegundulika madini yasiyopatikana katika kila nchi.

“Kwa sisi ambao tunaweza kudadisi siasa za Afrika tangu uhuru, ndivyo inavyofanyika katika nchi ambazo zinagundua rasilimali, kwa sababu tukiungana, hakuna mtu atachukua gesi, makaa ya mawe, chuma na ukiangalia nchi masikini ambazo hazina rasilimali hazijawahi kugawanyika.

“Ndiyo maana kuna maeneo muhimu ambayo yanalengwa, yanaweza kuwagawa watu, nchi inaweza kugawanyika watu wakiwa na makovu yasiyotibika, imani za watu kutengenezewa wananchi na vyombo vyao vya ulinzi na usalama, ni rahisi sana kugonganishwa,” alisema. 

 Aliwaomba Watanzania kutoingia katika mtego wa kukosa tumaini dhidi ya vyombo vya usalama, ambavyo vinafanya kazi kubwa ikiwemo kuzuia vurugu zilizowahi kutokea Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Waziri Mkuu, alisema Watanzania wanatakiwa kukataa jaribio lolote, ambalo linaelekeza kuwasha moto na kuharibu uchumi wa nchi yao.

“Vijana wa Tanzania tuilinde nchi yetu, imeshaundwa Wizara ya Vijana ambayo kazi yake ni kushughulikia masuala ya vijana na watafikiwa,” alisema.

Pia, Dk. Mwigulu, aliwataka Watanzania kuungana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuiamini Tume ya Uchunguzi, inayoongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande, ambayo iliundwa kuchunguza vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi kupata uhalisia wa kilichotokea.

Alisema kwa kuwa kila mtu analizungumzia lililotokea, ni muhimu kuiamini Tume hiyo, ambayo ina watu wanaoheshimika nchini, Afrika na duniani na waliobobea katika masuala ya sheria na haki.

Alitoa pole kwa familia zote zilizopotelewa na wapendwa wao katika vurugu hizo, akisema katika imani yake, kumwaga damu ya mtu mmoja asiye na hatia, siyo baraka katika ardhi husika.

Alitoa wito kwa kila mwananchi kwa dhamira yake, kunuia jambo la aina hiyo lisitokee tena nchini, kwa kuwa siyo baraka, linatengeneza makovu yasiyopona na linatupa gharama.

WATAKAOKIUKA MAADILI

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu alisisitiza serikali haitasita kumfukuza kazi mtumishi wa umma, ambaye atakiuka maadili ya kazi.

Dk. Mwigulu, alisema mtumishi mzembe, mla rushwa, asiye na nidhamu, atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Alisema serikali imeanza kuweka msimamo wa uwajibikaji, kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchauzi ya CCM na Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050, inayolenga maisha ya Watanzania.

“Tunatambua ndani ya Serikali tuna watumishi wa umma wazuri, ndiyo maana nchi imepiga hatua, lakini wapo wadokozi wanaotekeleza miradi chini ya kiwango na wala rushwa.

“Hawa ndiyo tumesema tutashughulika nao, nimeelekeza mtumishi mzembe, mla rushwa asihamishwe kituo, akishathibitishwa, afukuzwe kwa sababu, hatuna uhaba wa vijana wa kitanzania ambao wanaweza kufanya kazi kwa uaminifu na ukamilifu,” alisema Dk. Mwigulu.

Previous Post

SIMBA YAPEWA MCHONGO

Next Post

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

Next Post
DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUMEJIPANGA AFCON 2027

TUMEJIPANGA AFCON 2027

4 months ago
MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?