• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIMAMIENI HAKI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SIMAMIENI HAKI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH, Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa majaji na mahakimu nchini, kusimama katika mstari wa haki pindi wanapotoa uamuzi, akisisitiza uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu ya utawala bora na msingi wa upatikanaji haki.

Amesema wajibu wa majaji na mahakimu ni kusimamia haki kwa kuzingatia katiba, sheria, maadili, bila hofu, huba na upendeleo.

Dk. Samia aliyasema hayo Dodoma, katika hotuba ya ufunguzi mkutano mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) ambapo alisisitiza utulivu wa Tanzania ni muhimu kwa watoa haki.

 “Ni jukumu lenu pia  kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi yetu. Ni muhimu kwa watoa haki nchini, kusimama katika mstari wa haki mnapofanya maamuzi ya kutoa haki.  

 “Hakuna Taifa lenye maendeleo endelevu na ustawi wa watu wake bila usimamizi mzuri wa haki. Uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu ya utawala bora na upatikanaji haki.

“Serikali itaendelea kulinda uhuru wa mahakama. Uhuru huo hauna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu,nidhamu, utii wa sheria na uzalendo kwa taifa letu,”alisema. 

Rais Samia, alisema majukumu ya majaji na mahakimu ni mazito, kwani yanahitaji weledi, busara na uaminifu katika kusimamia haki bila uoga na upendeleo.

“Kuna watu wanafungwa kwa kesi za kusingiziwa, sasa mambo gani yamepita huko mpaka anapewa kesi ya kubambikiwa, akitoka huko anasema sikuwa na kesi, nimebambikiwa tu lakini nimekaa (gerezani) nimetoka.

 “Wewe uliyemnyima uhuru wake, ukamfanya aende kufungiwa, jipime una jukumu gani?,” alisisitiza..

 Alisema imani ya Watanzania kwa mahakama imeendelea kuongezeka jambo ambalo linatia moyo kwamba, mahakama inafanya kazi zake inavyoridhisha.

“Serikali ya Awamu ya Sita, imeendelea kuchukua hatua kuimarisha mazingira ya mahakama ikiwemo majengo, kuongeza rasimiliamali watu kuanzia majaji na mahakimu,” alieleza.

MASLAHI YA MAJAJI NA MAHAKIMU

Katika hotuba yake, Dk. Samia, aligusia suala la maslahi kwa majaji na mahakimu ambapo alieleza namna ambavyo serikali inavyoendelea kuboresha maslahi yao kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti.

“Nataka niwaibie siri, napata barua za kuboresha maombi na maslahi. Naambiwa kama walivyo majaji na sisi tunataka tuwe kama hivyo. Suala la bajeti inategemea hali ya ukuaji uchumi wa Tanzania, tunagawana kwa kile kilichopo.

“Jinsi tunavyofanyakazi na haki ikapatikana mapema, ndivyo uchumi  Watanzania unavyokuwa.

“Uchumi unavyokuwa ndivyo tutaangalia mgawanyo wa rasilimali kwa mihimili yetu. Kwa miaka mitano iliyopita, uchumi wetu umekuwa ukikua hatua kwa hatua na hatujawahi kurudi nyuma, jinsi tunavyokua ndivyo bajeti itakavyokua,” alibainisha.

Rais Dk. Samia alisema serikali imefanya kazi kubwa kufanya maboresho katika muhimili huo.

 “Katika hili la mishahara huku serikalini tunapimwa kwa mishahara, hata tunapopanga bajeti zetu, tunakaguliwa na mashirika makubwa ya kimataifa, siyo kwamba hatutaki kuwafanya watu wote kupata mishahara itakayowawezesha waishi vizuri, lakini kuna kikomo.

 “Lakini, tumejitahidi kwa kile tunachokipata tunaongeza mishahara.

Uwezo ukiruhusu tutafika huko lakini kama uwezo hautaruhusu twendeni polepole sisi bado nchi inayoeendelea.

“Bado kuna mambo mengi ya kufanya katika sekta mbalimbali, namna tunavyokuwa tutaongeza stahiki na mishara ya majaji na mahakimu,”alisema.

 Alisema kwa yale mapendekezo kuhusu mabadiliko ya sheria na masuala mengine ambayo hayahitaji rasilimali fedha, yatakwenda kufanyiwa marekebisho  majaji na mahakimu wafanyekazi zao vizuri.

MIFUMO YA TEHAMA

Rais Dk. Samia ambaye ameingia katika rekodi ya kuwa Rais wa pili kuhutubia mkutano huo akitanguliwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1984, alisema serikali imeimarisha vyema matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Alisema mifumo ya TEHAMA, inatumika vizuri katika utendaji wa haki nchini akitolea mfano uwepo wa mfumo wa kieletroniki unaoonyesha idadi ya kesi na jaji anayeshughulikia.

“Siku nilipokuja kuzindua hili jengo (Mahakama Kuu), nilitembezwa kuna ‘dashboard’ inayoonesha orodha ya kesi, jaji aliyepangiwa na hukumu iliyotoka. Hakuna mfumo huo maeneo mengine, tunao sisi Tanzania. Nchi yenye mfumo huo, naambiwa ni Kazakhistan ambayo wenyewe walikuja kutungalia sisi tunavyofanya.

“Tunapochukua hatua hizi, tunalenga kuwa mhimili wa haki wa kisasa wenye huduma bora, zinazopatikana kirahisi, kwa wakati na kwa ufanisi,”alisisitiza.

MAHAKAMA NA DIRA 2050

Rais Dk. Samia, alisema Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025/2050 imejengwa katika misingi ya utawala bora, usalama, amani na utulivu.

Alisema Taifa linapokwenda kutekeleza dira hiyo, mhimili wa mahakama una nafasi muhimu kujenga nchi yenye haki, amani, usalama na utulivu.

“Dira 2050 inatambua utawala bora na utawala wa sheria ni msingi wa maendeleo endelevu, jambo hili haliwezekani pasi uwepo wa mahakama imara yenye kuaminika na wananchi. Nasi serikali tunaelekea kujenga mahakama hiyo.

“Nataka niwaambie, serikali tulipitisha mpango wa muda mrefu wa utekelezaji Dira 2050 ambapo katika mpango ule asilimia 22 ya mambo yatafanywa na serikali, asilimia 70 yatafanywa kwa ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi.

Kwa mujibu wa Dk. Samia: “Asilimia nane yatafanywa na mashirika yetu ya umma katika hali kama hiyo, mahakama ina kazi kubwa ya kufanya kwa sababu tunategemea isimame imara kwani tunatarajia kualika sekta binafsi kuja Tanzania.”

Alisema kutaibuka migogoro mbalimbali ya kazi, kodi na utekelezaji wa mikataba, hivyo mahakama itategemewa kutetea haki ya Watanzania.

HUKUMU KWA KISWAHILI

Kwa upande wake, Mlezi wa TMJA, Jaji Mkuu George Masaju, alisema mahakama, itaanza kuandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili pindi Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakapokamilisha tafsiri ya matoleo ya kisheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili.

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakapokuwa amekamilisha tafsiri ya matoleo ya kisheria kwa lugha ya Kiswahili, tutaanza kuandika hukumu kwa Kiswahili. Nimeambiwa yuko katika hatua za mwishoni,”alieleza.

Alibainisha kuwa, matumizi ya Kiswahili katika nyaraka na hukumu za mahakama yatasaidia kuongeza uwazi, kuimarisha imani ya wananchi pamoja kurahisisha utekelezaji uamuzi wa mahakama nchini.

UCHELEWESHAJI HAKI

Kuhusu utoaji haki, Jaji Mkuu Masaju alitoa wito kwa majaji na mahakimu kutochelewesha haki bila sababu za msingi.

 “Mambo yanayoweza kusababisha labda uchache wa watendaji na mahakimu, kitu ambacho serikali imepiga hatua kubwa sana kujitosheleza kwa idadi ya majaji na mahakimu, ingawa bado hatujafika, lakini ukiangalia ilivyokuwa huko nyuma tumepiga hatua,” alisisitiza.

Alisema mahakama imejipanga kuja na utaratibu wa kusikiliza na kuamua kesi kwa haraka zaidi.

Jaji Mkuu Masaju, alisema mabadiliko hayo, yanatokana na hatua kubwa iliyopigwa na serikali katika kuongeza idadi ya majaji, mahakimu na kuboresha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).  

KAULI YA RAIS TMJA

Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Elimo Massawe, alisema uwepo wa Rais Dk. Samia katika mkutano huo, umeonesha wazi dhamira ya serikali anayoiongoza katika kuimarisha uhuru wa mahakama nchini.

Alisema malengo makuu ya chama hicho chenye wanachama zaidi ya 1,700 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ni kukuza na kulinda uhuru wa mahakama, kukuza maslahi na ustawi wa wanachama, kusimamia hadhi, heshima na tamaduni za majaji na mahakimu.

Massawe, alisema malengo mengine ni kuongeza maarifa na ujuzi wa majaji pamoja na mahakimu, kutoa taarifa za machapisho kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu wanachama, kushirikiana na kujiunga katika vyama au taasisi nyingine zenye malengo yanayofanana.

Previous Post

DRC WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUTOA HIFADHI YA WAKIMBIZI

Next Post

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

Next Post
‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

1 day ago
DK. SAMIA ATEUA, ATENGUA VIGOGO

DK. SAMIA ATEUA, ATENGUA VIGOGO

4 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?