• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DRC WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUTOA HIFADHI YA WAKIMBIZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 14, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
DRC WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUTOA HIFADHI YA WAKIMBIZI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

UJUMBE wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ukiongozwa na Waziri wa Nchi, anayeshughulikia masuala ya Ustawi wa Jamii, Hatua za Kibinadamu na Mshikamano, Bazaiba Masudi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutoa hifadhi ya wakimbizi kutoka nchini DRC katika hali ya utu na amani kwa takribani miaka 30 tangu kuanzishwa kwa kambi hiyo.

Aidha, amewaeleza kuwa Serikali ya DRC inaendelea na jitihada za kutafuta suluhisho la kuleta amani ya kudumu ili waweze kurejea nchini kwao.

Pia amewasihi kuishi kwa nidhamu na maadili ili kuilinda heshima ya DRC na kuthamini ukarimu wa Serikali ya Tanzania.

Bazaiba ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.

Bazaiba ametembelea kujionea maisha ya Wakimbizi wa DRC katika kambi hiyo na kusikiliza maombi na mapendekezo yao kwa Serikali ya DRC.

Amewataka Wakimbizi walio tayari kurejea nyumbani kuendelea kujiandikisha rasmi ili waweze kurejea kwenye makazi yao na kufanya shughuli za maendeleo, mambo ambayo hawawezi kufanya wakiwa kambini.

Naye, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, James Millya (Mb) amewaeleza wakimbizi hao kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kusimamia misingi ya Sheria za Kimataifa za uhifadhi wa Wakimbizi hivyo, itaendelea kushirikiana nao katika kipindi chote wawapo nchini pamoja na kuwahakikishia usalama wao katika mchakato mzima wa kurejea nchini kwao.

Aidha, ameeleza kuwa zoezi la kurejea nyumbani ni la hiari na si shuruti.

Akiwasilisha taarifa ya kambi, Kaimu Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu, Samwel Kuyi ameeleza kuwa kambi ina jumla ya wakimbizi 132,404. Wakimbizi 86,918 ni kutoka DRC, 45,346 ni Warundi na 98 kutoka mataifa mengine. Zaidi ya 60% ya wakimbizi wa DRC ni watoto chini ya miaka 18 kati yao 21,660 ni watoto chini ya miaka mitano.

Moja ya wakimbizi, Apolina Masumbuko amesema wako tayari kurejea nyumbani na kuomba Serikali ya DRC iweze kurejesha amani nchini kwao ili warudi katika mazingira salama na tulivu.

Previous Post

ROONEY KUREJEA MAN UNITED

Next Post

SIMAMIENI HAKI

Next Post
SIMAMIENI HAKI

SIMAMIENI HAKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DIARRA, LOEMBA, OURA WALIVYOTIKISA DABI YA K’KOO

DIARRA, LOEMBA, OURA WALIVYOTIKISA DABI YA K’KOO

2 months ago
DK. NCHIMBI ATAJA SULUHU FOLENI DAR

DK. NCHIMBI ATAJA SULUHU FOLENI DAR

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?