• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBASC NJIA HII HAPA MAKUNDI KIMATAIFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 3, 2025
in Burudani, Michezo
0
SIMBASC NJIA HII HAPA MAKUNDI KIMATAIFA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA

LICHA ya kuanza vibaya katika kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu huu, Simba bado ina nafasi ya kutinga robo fainali kama tu itachanga vyema karata zake kimahesabu katika mechi nne zilizobakia.

Wekundu hao wa Msimbazi waliopangwa kundi moja na Petro Atletico ya Angola, Esperance ya Tunisia na Stade Malien kutoka Mali, imeanza kwa kufungwa katika mechi zake mbili ilizocheza.

Miamba hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam, ilianza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Petro Atletico nyumbani kabla ya mwishoni mwa wiki kukubali kupoteza mabao 2-1 ilipochuana na Stade Malien ugenini.

Kutokana na matokeo hayo, hivi sasa Simba ili kufufua matumaini ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo, inapaswa kuvuna angalau pointi 10 au 12 katika mechi nne zilizobaki.

Katika mechi zilizobakia zitakazopigwa kuanzia Januari mwakani, Simba itacheza mara mbili na Esperance (nyumbani na ugenini), Petro ugenini kabla ya kumalizana na Stade Malien nyumbani.

Katika mchanganuo wa pointi, ili Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe alama 10 wanapaswa kushinda mechi tatu na kutoka sare moja kati ya mechi nne au kushinda zote ili kufikisha alama 12 kuwa na asilimia kubwa ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo msimu huu.

Tangu ilipofuzu hatua ya makundi ya CAFCL msimu wa 2018/2019, Simba haijawahi kushindwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa msimu wowote iliyotinga makundi.

Akizungumzia hali ya hivi sasa ya kikosi chao, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema wana muda wa kutosha kujipanga kwa mechi zilizobaki kuhakikisha wanatinga robo fainali.

Ahmed alisema hadi kufikia katika mechi hizo, timu hiyo itakuwa imefanyiwa marekebisha makubwa kuhakikisha inatinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Mechi yetu ya tatu ya hatua ya makundi tutacheza Januari 21, 2026 dhidi ya Esperance ugenini. Kutoka leo (juzi) hadi Januari 21 ni siku zaidi ya 50.

“Katika siku hizo kikosi chetu kitafanyiwa mabadiliko makubwa ya kiufundi na itakapobidi kuongeza nguvu katika dirisha dogo tutafanya hivyo na tunaamini mabadiliko hayo yataturejeshea makali yetu.

“Umefika ule muda wa Simba yetu kuonyesha maajabu yake na kuwashangaza watu, kwa hivi sasa tunaanza maandalizi ya michezo yetu ya Ligi Kuu Bara. Tukumbuke kuwa katika ligi tuna mwenendo mzuri hivyo tunapaswa kuwekeza nguvu kubwa tusiteleze,” alisema.

Katika Ligi Kuu Bara, Simba inakabiliwa na kibarua dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kesho kabla ya kuchuana na Azam FC.

Katika msimamo wa michuano hiyo, Simba ipo nafasi ya saba kwa alama tisa baada ya kupata ushindi katika mechi zote tatu ilizocheza, ikifunga mabao manane na kuruhusu bao moja.

Wekundu hao wa Msimbazi wameshinda mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate, 3-0 dhidi ya Namungo na 2-1 ilipochuana na JKT Tanzania.

Previous Post

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

Next Post

AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

Next Post
AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA USIPIME SHINYANGA

DK. SAMIA USIPIME SHINYANGA

6 months ago
YANGA YAKUBALI YAISHE

YANGA YAKUBALI YAISHE

2 months ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?