• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home MAKALA MICHEZO

MAJIJI SITA MOROCCO KUIPAMBA AFCON

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 15, 2025
in MAKALA MICHEZO
0
MAJIJI SITA MOROCCO KUIPAMBA AFCON
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA

MASHINDANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, yanatarajiwa kufanyika Alhamisi hii hadi Januari 18, mwakani nchini Morocco.

Fainali hizo za 35 za michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika, zinatarajiwa kupigwa katika majiji sita tofauti nchini Morocco.

Majiji hayo ni Casablanca, Rabat, Marrakesh, Agadir, Fez na Tangier.

Katika maeneo hayo sita, jumla ya viwanja vya soka tisa vitatumika katika michuano hiyo.

CASABLANCA

Mji huo mkubwa zaidi katika nchi hiyo na kituo kikuu cha biashara na uchumi wa taifa hilo, unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa zaidi kwa wageni katika michuano hiyo.

Katika jiji hilo, kuna uwanja mmoja wa soka ambao utatumika katika michuano hiyo ambao ni Stade Mohammed V ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 45,000.

AGADIR

Katika jiji hilo, kutakuwa na uwanja mmoja ambao utatumika katika fainali hizo ambao unaitwa Adrar wenye uwezo wa kuingiza mashabiki wa soka 45,000.

FEZ

Katika jiji hilo lililopo Kaskazini mwa Morocco, uwanja utakaotumika katika fainali za AFCON ni Fez wenye uwezo wa kuingiza mashabiki wa soka 45,000.

MARRAKESH

Marrakesh ni jiji la nne kwa ukubwa nchini Morocco ambapo jiji hilo lipo magharibi mwa milima ya Atlas.

Katika jiji hilo, Uwanja wa Marrakesh ndiyo utatumika katika fainali hizo ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 45,000.

RABAT

Rabat ndiyo mji mkuu wa Morocco na jiji la saba kwa ukubwa nchini humo.

Katika jiji hilo, kuna viwanja vinne vya soka ambavyo vitatumika katika fainali za AFCON mwaka huu.

Viwanja hivyo ni Prince Moulay Abdellah wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 68,700, Moulay Hassan unaoingiza mashabiki 22,000, Rabat Olympic unaoingiza mashabiki 21,000 na Al Medina unaoingiza mashabiki 18,000.

TANGIER

Tangier ni jiji lililopo Kaskazini Magharibi mwa Morocco, katika pwani ya bahari ya Mediterranean na Atlantic.

Katika jiji hilo, uwanja wa Tangier Grand ndiyo utatumika katika fainali hizo, ambapo dimba hilo lina uwezo wa kuingiza mashabiki 75,600.

MAKUNDI

Michuano hiyo inayoshirikisha timu 24, jumla ya makundi sita yamepangwa ambapo kila kundi limehusisha timu nne.

Kundi A linaundwa na mwenyeji Morocco pamoja na timu za Mali, Zambia na Comoros wakati kundi B likiwa na Misri, Afrika Kusini, Angola pamoja na Zimbabwe huku kundi C lina timu za Tanzania ‘Taifa Stars’, Nigeria, Tunisia na Uganda.

Senegal inaunda kundi D na timu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Benin na Botswana wakati Algeria ipo kundi E na timu za Burkina Faso, Guinea ya Ikweta na Sudan huku kundi F likiwa na bingwa mtetezi Ivory Coast na timu za Cameroon, Gabon na Msumbiji.

Previous Post

NI SAFARI YA MABILIONI YA FEDHA AFCON 2025

Next Post

UNDANI WA KUNDI LA STARS AFCON 2025

Next Post
UNDANI WA KUNDI LA STARS AFCON 2025

UNDANI WA KUNDI LA STARS AFCON 2025

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

7 months ago
HERI YA 2026, AMANI NDIYO MPANGO MZIMA

HERI YA 2026, AMANI NDIYO MPANGO MZIMA

4 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?