• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 15, 2025
in Habari, Kitaifa
0
SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya viongozi na watumishi wa umma watakaoshindwa kujaza na kuwasilisha kwa wakati fomu za tamko la maadili katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Rais Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Zanzibar, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, kila kiongozi na mtumishi wa umma anatakiwa kuwasilisha fomu hizo kabla ya tarehe 30 Desemba 2025.

Akielezea taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Rais Dk. Mwinyi amesema kuwa hadi sasa ni viongozi 530 pekee, sawa na asilimia 19, kati ya viongozi 2,750 wanaotakiwa kisheria, ndio waliokamilisha zoezi hilo. Ameeleza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya watakaokiuka matakwa hayo ya kisheria.

Katika hatua nyingine, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ipo katika maandalizi ya kuanzisha Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Viongozi, utakaolenga kuongeza uwajibikaji, ufanisi na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha utendaji wa taasisi za umma.

Akizungumzia mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi, Rais Dk. Mwinyi amesema Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi (ZAECA) imepokea na kufanyia kazi jumla ya taarifa 524.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2025, ZAECA imefanikiwa  kidhibiti na kuokoa Jumla ya Shilingi 6,426,282,551/= na dola za kimarekani (USD) 89,371 zilirejeshwa Serikalini na shilingi 1,143,487,556/= na dola za Kimaekani (USD) 4,999 zilirejeshwa kwa wananchi.

Rais Dk. Mwinyi amesema Tanzania, ikiwemo Zanzibar, imeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Malengo ya Umoja wa Mataifa yanayohusiana na haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa, kupitia uridhiaji na utekelezaji wa mikataba na mikakati ya kimataifa.

Akihitimisha hotuba yake, Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa viongozi wa taasisi za Serikali kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli na maendeleo ya nchi, na pia kuhimiza wananchi, vyombo vya habari, asasi za kiraia na sekta ya umma kushirikiana na Serikali katika kuimarisha utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa.

Vilevile, Rais Dk. Mwinyi ameipongeza Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu uvunjaji wa maadili ya viongozi, ambapo jumla ya malalamiko 28 yalipokelewa na manane tayari yamefanyiwa kazi.

Previous Post

MAADILI KAZINI YAWE MSINGI WA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI – NDEJEMBI

Next Post

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

Next Post
TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

“Wasichana milioni mbili wanufaika na elimu ya stadi za maisha

8 months ago
WAZIRI NANAUKA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA SHUGHULI ZA VIJANA

WAZIRI NANAUKA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA SHUGHULI ZA VIJANA

5 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?