• ePaper
Friday, May 1, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAADILI KAZINI YAWE MSINGI WA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI – NDEJEMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 15, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MAADILI KAZINI YAWE MSINGI WA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI – NDEJEMBI

WAZIRI wa Nishati, Deogratias Ndejembi

0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WATUMISHI katika Wizara ya Nishati wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania, hususan kwa kujiepusha na vitendo vya rushwa, ubadhirifu na uzembe mahali pa kazi.

Waziri wa Nishati, Deogratias Ndejembi, ameyasema hayo Desemba 15, 2025, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mkoani Morogoro.

Akizungumza katika mkutano huo, Ndejembi amesema  maadili ya kazi ni nguzo muhimu katika kukuza sekta ya nishati na kuharakisha
maendeleo ya Taifa, akibainisha kuwa nishati ikiwemo umeme, mafuta na gesi ni mhimili mkubwa wa uchumi wa nchi.

“Zingatieni maadili kazini katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kujiepusha na vitendo vya rushwa, ubadhirifu na uzembe mahali pa kazi,
ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za umeme, mafuta na gesi,” amesema Ndejembi

Aidha, amewataka watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi ili kuendelea kuchochea maendeleo ya sekta ya nishati na kukuza uchumi wa Taifa.

Kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika, amesema Wizara ya Nishati ina jukumu la kuhakikisha Tanzania inazalisha jumla ya megawati 8,000 za umeme ifikapo mwaka 2030 kupitia vyanzo mchanganyiko, ikiwemo utekelezaji wa miradi mipya ya uzalishaji umeme.

Ameongeza kuwa katika kufikia lengo hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuweka vipaumbele sahihi vya nishati  ili kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa wakati.

Vilevile, amewataka watendaji wa Wizara kupitia Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia kuendelea kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia  kwa wananchi ili kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, kama ilivyoainishwa katika Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema Wizara itaendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya umeme, gesi na mafuta ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za nishati zilizo bora, salama na za uhakika.

Previous Post

MAHAKAMA ZANUFAIKA NA MAGEUZI YA TEHAMA

Next Post

SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

Next Post
SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

SMZ KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI AMBAO HAWATAWASILISHA FOMU ZA MAADILI KWA WAKATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UFAULU MITIHANI KIDATO CHA II, DARASA LA NNE WAONGEZEKA

UFAULU MITIHANI KIDATO CHA II, DARASA LA NNE WAONGEZEKA

4 months ago
PANTEV KICHEKO SIMBASC

PANTEV KICHEKO SIMBASC

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?