• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 1, 2026
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Taifa Stars ilitinga hatua hiyo kwa kanuni ya ‘best looser’ baada ya kumaliza kundi C la michuano hiyo ikiwa nafasi ya tatu kwa alama mbili kufuatia juzi kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia.

Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dk. Samia aliimwagia sifa miamba hiyo kwa kuandika historia hiyo kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka Afrika.

“Ninaipongeza timu yetu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya AFCON kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.

Heshima hii kubwa kwetu ni matokeo ya maandalizi mazuri na kujituma kwenu katika kila mchezo. Mmeandika historia kubwa kwa Taifa letu na mmeleta furaha kwa Watanzania wote. Hongereni sana,” aliandika Dk. Samia.

Rais pia, aliitakia kila la kheri Taifa Stars katika mchezo wa hatua hiyo dhidi ya Morocco utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah jijini Rabat, Morocco.

Naye Makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, alimuunga mkono Rais Samia kwa kuipongeza Taifa Stars kutinga hatua ya 16 bora.

“Ninaungana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuipongeza Taifa Stars kwa kufikia mafanikio ya kihistoria ya kufuzu hatua ya 16 bora katika AFCON. Tunawatakia kila la kheri katika michezo inayofuata,” Dk. Nchimbi alitoa pongezi hizo kupitia mtandao wa Instagram.

Katika kundi C, Taifa Stars ilikuwa chini ya kinara Nigeria yenye alama tisa na Tunisia pointi nne na juu ya Uganda iliyoburuta mkia kwa pointi moja.

Tanzania ilianza michuano hiyo kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Nigeria kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda na 1-1 ilipocheza naTunisia. 

Previous Post

NDOTO YATIMIA

Next Post

TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI

Next Post
TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI

TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

8 months ago
RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

4 weeks ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KAMILI AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?