• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 1, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SULEIMAN JONGO,
Karatu

MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Shadrack Mziray ameeleza mafanikio makubwa ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Awamu ya Nne (TPRP IV) uliokamilika Desemba 2025.

Amesema mradi huo wa kimkakati umefanikiwa kutekelwza miradi mingi ambayo imekuwa mkombozi kwa jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Karatu mkoani Arusha, Mziray amesema mradi huo umechangia kwa kiwango kikubwa kuendeleza ajenda ya maendeleo ya taifa, hususan kupunguza umaskini, kuboresha huduma za kijamii, na kuwezesha jamii nchini.

“Tangu kuanza kwa mradi huu Januari 2020, TPRP IV imejikita kimkakati katika kupunguza umaskini katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Njombe, Geita na Simiyu.

“Lengo kuu lilikuwa kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii na fursa za kuongeza kipato, hii imefanyika kwa kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu lengwa, mradi umewezesha ujenzi na ukarabati wa madarasa, vituo vya afya na vyanzo vya maji ambavyo sasa vinahudumia kaya za walengwa pamoja na jamii kwa ujumla.

“Uwekezaji huu umeongeza upatikanaji wa huduma, umepunguza umbali wa kufikia huduma za afya na maji, na kuimarisha mazingira wezeshi kwa ustawi wa jamii. Mradi pia umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ustahimilivu wa kiuchumi,” amesema.

Akieleza zaidi amesema kaya zilisaidiwa kutanua wigo wa vyanzo vya kipato kupitia shughuli kama ajira binafsi katika sekta mbalimbali ikiwemo za kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za uzalishaji.

Amefafanua matokeo yake, familia nyingi zimeongeza kipato cha kaya, kuboresha usalama wa chakula na kuimarisha uwezo wa kukidhi mahitaji ya msingi.

“Tathmini za hivi karibuni zinaonesha kuwa mradi huu (TPRP IV) umenufaisha kaya takriban 200,007 kwa kiwango cha mwitikio wa asilimia 96.7, jambo linaloonesha wigo mpana na athari chanya za afua za mradi.

“Mojawapo ya mafanikio makubwa ni kukuza usawa wa kijinsia na kuunga mkono elimu ya wasichana. Ujenzi wa mabweni, vyoo na madarasa umeongeza uandikishaji, kuboresha udumishaji wa wanafunzi shuleni, na kupunguza mimba za utotoni,” ameleza.

Pia, amesema hatua hizo zimechangia kuboresha matokeo ya kielimu na kuongeza fursa kwa wasichana. Msisitizo wa ushirikishwaji wa jamii umejenga uwajibikaji wa pamoja na uendelevu, kuhakikisha rasilimali zinaendelea kufanya kazi na kutunzwa hata baada ya mradi kukamilika.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

Next Post

MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

Next Post
MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA ATANGAZA HATUA ZA MWISHO UTEKELEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

DK. SAMIA ATANGAZA HATUA ZA MWISHO UTEKELEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

7 months ago
WASANII WASHUSHA BURUDANI NZITO MIKUTANO YA KAMPENI ZA DK. SAMIA

WASANII WASHUSHA BURUDANI NZITO MIKUTANO YA KAMPENI ZA DK. SAMIA

8 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?