• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 1, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeendelea kuvunja rekodi ya ukusanyaji mapato, baada ya kusanya sh. trilioni 9.8 kuanzia Oktoba hadi Desemba, mwaka jana.

Pia, imeandika historia mpya ya kukusanya sh. trilioni 4.130 mwezi Desemba pekee, ikilinganishwa na sh. trilioni 3.5 zilizokunywa kipindi kama hicho mwaka 2024.

Aizungumza Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesema ukusanyaji wa sh. trilioni 9.8 umevuka lengo lililokusudiwa ambalo ni sh. trilioni 9.6.

“Tulipaswa kukusanya shilingi trilioni tisa na bilioni 660, lakini tumekusanya shilingi trilioni tisa na bilioni 800, hiki ni kiasi kikubwa ni ufanisi wa asilimia 101.2 ,”amesema Kamishna Mwenda.

Kamishna Mwenda alisema Desemba mwaka jana, waliweka lengo la kukusanya sh. trilioni 4.14, lakini walivuka lengo na kufikia trilioni 4.130 mafanikio ambayo hayakuwahi kutokea tangu kuanzishwa mamlaka hiyo.

“Kiasi hiki ni kikubwa ni mara ya kwanza hakijawahi kukusanywa na TRA kwa mwezi mmoja, mwaka jana mwezi kama huo (Desemba 2024) tulikusanya shilingi trilioni tatu na bilioni 500,”amesema.

Vilevile Kamishina Mwenda alisema, wastani wa ukusanyaji kodi kwa mwezi umepanda kutoka sh. trilioni 2.7 hadi sh. trilioni 3.130 kwa mwezi.

Kamishina Mwenda alisema mafanikio hayo yametokana na uhimilivu wa uchumi uliopo  nchini, sera za uchumi, ulipaji kodi kwa hiyari na mfumo mzuri wa kodi uliowekwa.

Pia, Kamishina huyo alitaja sababu nyingine zilizochangia mafanikio hayo ni jitihada za utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa TRA.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kujenga uchumi himilivu, mwezi Oktoba pamoja na changamoto hatukushuka kiwango tulichotakiwa kukusanywa na mwezi Novemba hatukushuka,”ameongeza.

Aidha, Kamishna Mwenda amesema mwaka huu TRA imejipanga kusimamia sheria za kodi, kupambana na wakwepa kodi na kuendelea kusimamia uadilifu kwa watendaji wa mamlaka hiyo.

“Tutaimarisha sana watumishi wetu na kusimamia uadilifu katika utendaji kazi,”ameongeza.

Aidha Kamishina Mwenda amesema TRA imejipanga kuboresha huduma zake,ambapo inatarajia  kuanzisha mfumo mpya wa kodi za ndani utakao anza Januari mwaka huu.

“Kupitia mfumo huo mambo mengi yatafanyika ‘online’ ule usumbufu wa walipa kodi kwenda kwenye ofisi zetu utapungua sana.

“Tutakuwa na maamuzi ya kikodi ambayo ni ‘data base’ tofauti na awali,”amesema  Kamishna Mwenda.

Amesema mfumo huo utafanywa kidijitali hatua ambayo itarahisisha utendaji kazi, kuboresha huduma kwa walipa kodi na kuondoa malalamiko.

Kamishna Mwenda amesisitiza TRA itaendelea kushirikiana na walipa kodi kwa kuwezeha katika shughuli zao za biashara na kuendelea kuwasikiliza.

Vilevile, Kamishna Mwenda ametoa rai kwa wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiyari kwa mustakbali wa maendeleo ya taifa.

Previous Post

TASAF YABAINISHA MAFANIKIO MPANGO WA KUPUNGUZA UMASKINI

Next Post

GAMONDI AJA KIVINGINE KUIVAA MOROCCO AFCON

Next Post

GAMONDI AJA KIVINGINE KUIVAA MOROCCO AFCON

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AKOSHWA NA MAELFU YA WANANCHI WALIOJITOKEZA UWANJA WA SAMORA

DK. SAMIA AKOSHWA NA MAELFU YA WANANCHI WALIOJITOKEZA UWANJA WA SAMORA

8 months ago
DK. SAMIA AWAONYA WATU WENYE NIA OVU

DK. SAMIA AWAONYA WATU WENYE NIA OVU

7 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?