• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MAKONDA ATOA NENO AFCON 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 26, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
MAKONDA ATOA NENO AFCON 2027
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA 

WAZIRI  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ametoa neno kwa Watanzania kutoibeza nchi yao kwa sababu  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anafanya mambo mazuri yakiwemo maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ na kutunza amani ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam, katika pambano  la ‘Knockout  ya Mama’ msimu wa nane, lililofanyika Ukumbi wa Biashara na Usafirishaji wa Afrika Mashariki, Ubungo Dar es Salaam, alisema kuna baadhi ya watu wakiona AFCON 2027 inafanyika nchini wanaanza kuongea mambo mabaya juu ya taifa.

“Watanzania tunapaswa kuachana na tabia ya kuibeza nchi yetu kwani Rais Dk. Samia anafanya makubwa anatuletea michuano ya AFCON  mwakani, pia ‘Miss World’ itafanyika  hapa nchini.

“Mashindano haya yatadumu ndani  ya siku 28 kwa kufanyika mashindano  madogo madogo hadi fainali,” alisema.

Aidha, Waziri huyo alisema Watanzania wanapaswa kufahamu amani ndiyo kila kitu katika nchi, hivyo wanapaswa kuilinda na kuitunza.

“Amani itawale kwani ni silaha kubwa hapa nchini, pia kujiandaa na matukio  makubwa  ya kimataifa ambayo yatalitangaza taifa letu  vizuri na kupata fursa nyingi kupitia mashindano hayo,” alisema.

Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ametoa maagizo kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakikisha mchezo wa mieleka unafanyika kwa ustadi mkubwa.

Maagizo hayo ameyatoa juzi katika pambano la ‘Knockout ya Mama’ msimu wa nane uliofanyika Ukumbi wa Biashara na Usafirishaji wa Afrika Mashariki, Ubungo Dar es Salaam.

Makonda alisema BMT  inatakiwa kuhakikisha mchezo wa mieleka unafanyika hapa nchini huku idadi kubwa ya Watanzania wakishuhudia.

“Tanzania ina watu wenye  miili mikubwa, hivyo  miili yetu tuitendee haki, lazima kila mtu katika hii nchi awe na mchezo wake, hamasa kubwa tumeona katika ngumi tunaomba wasichoke waendelee kuwaleta mabondia kukuza vipaji, “alisema.

Waziri huyo alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa mwanamichezo namba moja kwa kugusa kila sekta ya michezo kuanzia soka,riadha, netiboli, ngumi, na michezo mingine amefanya hivyo.

“Nimetoa maagizo mengine kwa Kamisheni ya Ngumi ya Kulipwa (TPBRC),waende nchi nzima kutafuta vipaji na kutambulika na kupanda katika majukwaa makubwa kama haya.

Previous Post

BALOZI NCHIMBI ATAKA RAIA KUILINDA AMANI

Next Post

SIMBA, MLANDEGE NI KUFA AU KUPONA

Next Post
SIMBA, MLANDEGE NI KUFA AU KUPONA

SIMBA, MLANDEGE NI KUFA AU KUPONA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MGOMBEA Mwenza wa Urais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Butiama, mkoani Mara. (Picha na Abdurahman Jumanne)

BALOZI DK. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE

8 months ago
DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?