• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BALOZI NCHIMBI ATAKA RAIA KUILINDA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
BALOZI NCHIMBI ATAKA RAIA KUILINDA AMANI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu, Unguja

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa wakazi wa Dunga, Mkoa wa Kusini Unguja, kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, katika kuhakikisha amani inaendelea kushamiri nchini.

Balozi Nchimbi alitoa wito huo katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika eneo la Dunga.

Dk. Nchimbi aliwasihi kushirikiana na Serikali kwa njia ya kutoa taarifa mbalimbali kuhusu wahamiaji haramu, watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria, au wanaojihusisha na shughuli haramu kinyume na malengo ya ukaazi wao.

Makamu wa Rais alisema amani na umoja ni Tunu za Taifa, ambazo kila Mtanzania anapaswa kuzilinda. 

KUMUUNGA MKONO RAIS

Balozi Nchimbi aliwasihi wananchi wote kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuiletea nchi maendeleo ili kwa pamoja kufikia malengo ya kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

Halikadhalika, Makamu wa Rais alitoa rai kwa taasisi za serikali kuendelea kuwaamini na kuwapa Watanzania wazawa kazi za ujenzi, waendelee kupata uwezo wa kiteknolojia na kifedha.

Makamu wa Rais aliipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya uhamiaji, kwa kutoa kandarasi kwa Mtanzania mzawa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kati, Unguja.

Aidha, alisema Serikali imejikita katika kuimarisha huduma za uhamiaji kwa kuboresha vitendea kazi na miundombinu kwa ujumla.

Dk. Nchimbi aliongeza kuwa, Ujenzi wa Ofisi za Uhamiaji za Wilaya ni njia mojawapo ya jitihada za kufikia azma hiyo.

UBORESHAJI

Pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya majengo, Serikali imeweka mkazo katika utoaji wa mafunzo kwa watumishi, kusimamia stahiki za watumishi, na uboreshaji wa mara kwa mara wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji nchini.

Vilevile, alisema huduma za uhamiaji Zanzibar ni muhimu na chachu katika kukuza sekta ya biashara, uwekezaji na utalii, kwa kuzingatia ongezeko kubwa la wageni wanaoitembelea, hususan katika kipindi ambacho Serikali zote mbili zimejikita kukuza sekta ya utalii kufuatia uzinduzi wa Filamu maarufu ya Royal Tour.

MUUNGANO, MAPINDUZI

Makamu wa Rais alisema Mapinduzi ya mwaka 1964, yaliyoongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume yana historia kubwa kwa Zanzibar na watu wake.

Tangu wakati huo, Mapinduzi hayo yameijengea heshima kubwa Zanzibar na kuwapa Wazanzibari wigo mpana wa kufanya uamuzi kuhusu maisha yao na kujiletea maendeleo.

Pia, alisema Muungano umeimarisha zaidi umoja, mshikamano na kudumisha amani,  utulivu na kuchochea maendeleo kwa wananchi wote.

Alisema baada ya Mapinduzi na Muungano, huduma mbalimbali za jamii kama vile afya na elimu zilifunguka kwa wananchi wote.

Jengo hilo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kati limegharimu sh. bilioni 2.1.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AFUNGUA UCHUMI WA BAHARI

Next Post

MAKONDA ATOA NENO AFCON 2027

Next Post
MAKONDA ATOA NENO AFCON 2027

MAKONDA ATOA NENO AFCON 2027

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAGOLI AFUNGUKA SIMBASC

MAGOLI AFUNGUKA SIMBASC

5 months ago
ICHAGUENI CCM  – DK. MWINYI

ICHAGUENI CCM  – DK. MWINYI

6 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?