• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 14, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter


Na SELINA MATHEW, DODOMA

SERIKALI imewataka washiriki wa shindano la Miss World Tanzania kubeba taswira halisi ya Mtanzania kwa kuzingatia tamaduni, maadili na utu wanapoiwakilisha nchi kimataifa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kuelekea shindano hilo litakalofanyika Aprili 19, mwaka huu.

Makonda alisema mshiriki atakayechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World nchini Vietnam, anapaswa kuwa balozi wa heshima ya taifa, akisisitiza kuwa ushindani huo si wa urembo wa sura pekee bali unaangalia mchango wa mshiriki kwa jamii.

Alisema ni muhimu kwa washiriki kuonyesha nidhamu, kujiamini na kulinda maadili ya Kitanzania.

Aliwataka washiriki 20 wanaowania taji hilo kutokata tamaa na kuendelea kupambania ndoto zao, akibainisha kuwa wanawakilisha si familia zao tu bali taifa zima.

“Mashindano haya Tanzania imeshiriki kwa miaka 29 na safari hii ikiwa ni ya 30 tunatarajia kufanya vizuri zaidi. Aidha, mshiriki wetu anapaswa kutangaza Kiswahili, ambacho ni fahari ya Taifa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miss World Tanzania, Mustafa Hassanali, alisema mshindi wa mwaka huu atanufaika na zawadi mbalimbali ikiwemo tiketi ya ndege kwenda Vietnam, gari, sh. milioni 10 pamoja na mshahara wa sh. milioni mbili kwa mwaka mmoja.

Aliongeza kuwa, mshindi huyo atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World yatakayofanyika Septemba 2026 nchini Vietnam, huku akiahidi ushindani mkali na wa viwango vya juu mwaka huu.

Previous Post

YANGA UBABE UBABE

Next Post

ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

Next Post
ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

6 months ago
KATIBUBMkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), BalozibDk. Asha-Rose Migiro

CCM IMEJIPANGA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU – BALOZI DK. MIGIRO

9 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?