• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

UJUMBE WA KILAINI, ANNA ABDALLAH MWAKA 2026

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 1, 2026
in Makala
0
UJUMBE WA KILAINI, ANNA ABDALLAH MWAKA 2026
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU 

WADAU mbalimbali nchini, wametoa ujumbe kwa Watanzania na matarajio yao mwaka huu, wakisisitiza jamii kudumisha amani, umoja na mshikamano.

Pia, wametoa rai kwa Watanzania kuwa na hofu ya hofu ya Mungu na kutokubali kushawishiwa kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi ya watu binafsi.

Wito huo ulitolewa na makundi mbalimbali ya wanasiasa wakongwe, viongozi wa dini,  asasi za kiraia na wananchi walipokuwa  wakizungumza na UHURU kwa nyakati tofauti.

Mwanasiasa mkongwe Anna Abdallah, alisema mwaka huu ukawe  wa amani na furaha kwa taifa.

 “Tuna muda wa kuponya yaliyotokea na kuendeleza amani, umoja, mshikamano kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu,”alisema.

Pia, Anna aliwasisitiza Watanzania kuhakikisha mwaka huu wanautumia kuchapa kazi, ili kujiimarisha zaidi kiuchumi na kukuza vipato vyao.

Vilevile, alimpongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kujenga taifa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika mwaka jana.

Anna aliwataka Watanzania kuendelea kushirikiana na serikali katika kulijenga taifa.

“Tuendelee kuchapakazi na kumtia moyo Mheshimiwa Rais Dk. Samia, maana katika awamu zote za utawala nchi hii haijawahi kutokea mafanikio makubwa yanayofanyika kwa kipindi kifupi kama chini ya Rais Samia.”alisema 

WARIOBA

Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alitoa rai kwa wananchi kuendelea na juhudi za kuleta maendeleo, kuendeleza uzalendo na  kudumisha umoja na amani.

KATE KAMBA

Kwa upande wake Mwenyekiti Mstaafu  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba, alitoa rai kwa Watanzania kutumia kipindi cha mwaka huu, kutenda mambo kwa hofu ya Mungu na kufanya ibada.

Aidha, Kate alisema ni matarajio yake na maombi yake kwa Mungu mwaka huu utakuwa wa neema nyingi, ikiwemo mvua za kutosha zitakazosaidia kuongeza uzalishaji wa chakula.

Pia, Kate alitoa rai kwa Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kuchapa kazi kwa bidii, wakulima walime kwa juhudi ili kuongeza zaidi akiba ya chakula.

“Mwaka huu ni matarajio yangu na maombi yangu ukawe mwaka wa mafanikio tupate mvua za kutosha kusiwe na madhara, tukazalishe mazao ya kutosha, tujitahidi tufanye kazi kwa bidii,”alisema.

BAKWATA

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA ), Nuhu Mruma alisema  mwaka huu mpya wamejipanga kuwasaidia viongozi wa serikali kuleta amani na utulivu nchini.

Alisema mwaka huu uwe mwaka wa kheri na baraka katika Taifa na wananchi kwa ujumla.

 “Mahusiano mazuri yanajenga taifa lenye amani na utulivu, hivyo sisi viongozi wa dini tutajitahidi kumwomba Mungu alete kheri na nchi yetu kuendelea kuwa na amani ,”alisema.

MATAKA

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Taifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Khamisi Mataka alitoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha amani, maridhiano kwa usalama wa nchi.

Mataka alisema maridhiano yanajenga taifa imara na lenye kuwa na  maendeleo kwa watu wake.

Mataka alisema mwaka huu uwe mwaka wa maridhiano, utulivu, upendo na amani kwa watu wote.

Pia, alisema jamii inatakiwa kufungua ukurasa mpya kutoka katika fikra potofu ambazo hazijengi nchi.

“Tuachane na fikra potofu,tusonge mbele huku tukiwa na fikra nzuri na ambazo zinaambatana na maendeleo ya kweli nchini kwetu,”alisema.

Aidha, alisema nchi ikiendelea kuwa tulivu maendeleo mwaka huu yataonekana huku miradi ikizidi kusonga mbele.

ASKOFU KILAINI

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki  la Bukoba Methodius Kilaini, alisema mwaka huu ukawe wa kufanya mageuzi makubwa ya maendeleo ndani ya nchi.

Alisema mara nyingi jamii inaingia katika mwaka mpya ikiwa imebeba shida na mizigo ya mwaka uliopita, jambo ambalo siyo sahihi,  badala yake wasonge mbele kumwomba Mungu na kutafuta maendeleo.

Pia, Askofu Kilaini alitoa rai kwa Watanzania kujikita kufanya mambo chanya na kushirikiana na wakuu wa nchi kuleta maendeleo yenye tija kwa taifa.

 “Ni  muhimu kutazama mbele na kuleta matumaini mapya, kila mmoja afunguke na kuacha mambo yaliyopita tusonge mbele na kuleta maendeleo,”alisema.

WASOMI

Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi na Uongozi kutoka Chuo cha Mwalimu Nyerere, Dk. Philip Daninga, alisema anautazama mwaka 2026 wa mabadiliko ya kweli na hatua mpya katika kujenga taifa imara.

Alisema mwaka huu unapaswa kuwa wa kujitathmini, kubadilika na kusonga mbele badala ya kuendelea kuishi kwa mazoea.

Alisisitiza mwaka 2026 unatakiwa uwe wa tofauti, wa kujifunza kutokana na makosa na kuyatumia kama msingi wa mafanikio makubwa.

Kwa upande wa maendeleo ya taifa, Dk. Daninga alisema anatarajia uwe wa mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Alieleza ni matarajio yake wananchi wataweka mipango bora itakayowezesha taifa kusonga mbele, hivyo alihimiza kufanya kazi kwa bidii.

Pia Dk. Daninga alitoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu  na kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana mwaka jana yawe mara mbili mwaka huu.

Dk. Daninga alisema ni matarajio yake kuona mwaka 2026, ukiitambulisha Tanzania kama taifa la amani, lenye rasilimali nyingi na mazingira rafiki ya uwekezaji.

Alisema taifa linapaswa kujitangaza vyema duniani, kuonesha kuwa ni mahali salama pa kuwekeza, kufanya biashara na kuishi.

Aidha, katika sekta ya afya, Dk. Daninga alisema anaona mwaka 2026 kama fursa ya kuimarisha mafanikio yaliyopo kupitia uwekezaji katika teknolojia ya kisasa na wataalamu bingwa.

Alifafanua Tanzania imeanza kuaminiwa kama kitovu cha matibabu Afrika Mashariki na Kati, hatua inayochangia kukuza uchumi na kuiweka nchi katika ramani ya kimataifa ya utalii wa afya.

Kwa upande wa jamii na familia, Dk. Daninga anatarajia mwaka huu uwe wa ustawi wa mahusiano, afya ya akili na uwazi katika kutatua changamoto.

WAFANYABIASHARA

Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wadogo ‘Machinga’, Stephen Lusinde, aliishauri jamii kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi, huku akiwahimiza wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao za kujipatia kipato.

Pia, alisema matarajio yake makubwa mwaka huu, ni kuona serikali inaendelea  kusimamia majukumu yake na viongozi kutimiza yale waliyoahidi kwa wananchi.

“Nampongeza sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuanza kutimiza ahadi alizoahidi kwa wananchi , niwaombe wananchi kuendelea kuiamini na kuipa ushirikiano wa kutosha serikali,”aliongeza.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara Walemavu Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWADA), Jerome Chitumbi, aliishauri jamii kutumia mwaka mpya kumrudia Mwenyezi Mungu na kutokubali kushawishika na watu wanaohatarisha amani ya nchi.

“Niwaombe wananchi kumrudia Mungu na tujiepusha na ushawishi wowote ule ambao utahatarisha amani ya nchi yetu, tujikite kufanya shughuli za kutuletea maendeleo nchini,”alisema.

RSA

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), Nassor Mansour, aliwasihi madereva kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani, kuacha mazoea hasa kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Alisema mwaka huu unapaswa uwe wenye mabadiliko makubwa hivyo, aliwahimiza madereva kuacha kutumia vilevi vya aina yoyote badala yake, wanatakiwa kuweka umakini wanavyokuwa barabarani.

“Niwaombe madereva kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha mikoa mbalimbali nchini, kuwa makini na kufuata sheria na kanuni zinazotakiwa barabarani,”alisema.

Naye, Katibu Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tawi la Mzimuni, Mohamed Sihaba, aliishauri jamii kukaribisha mwaka kwa kusherehekea kwa amani, utulivu na kujiepusha kufanya vurugu.

Previous Post

UKIFUATA USHAURI HUU WA KITAALAMU ‘UTATOBOA’ 2026

Next Post

NDOTO YATIMIA

Next Post
NDOTO YATIMIA

NDOTO YATIMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA TAMBO  TU 

YANGA TAMBO  TU 

2 months ago
SIMBASC YAITA MASHABIKI KWA MKAPA

SIMBASC YAITA MASHABIKI KWA MKAPA

6 months ago

Popular News

  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?