• ePaper
Sunday, January 11, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 9, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kufanya mazungumzo ya pande mbili na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Yi na kukubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadili kwa kina masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kihistoria na kimkakati kati ya Tanzania na China, hususan katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu uliojengwa katika misingi ya kuheshimiana na kuaminiana kwa manufaa ya pamoja kama ulivyo asisiwa na waasisi wa mataifa hayo.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru Serikali ya China kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania, hususan katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya miundombinu, afya, elimu, nishati na viwanda.

Ameeleza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kuvutia uwekezaji, biashara na teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake, Wang Yi ameeleza utayari wa China wa kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika juhudi zake za maendeleo na kusisitiza kuwa China itaendelea kuwa mshirika wa kuaminika wa Tanzania na Afrika nzima katika kutekeleza ajenda za maendeleo ya pamoja, ikiwemo kupitia Mpango wa Ukanda wa njia (Belt and Road Initiative) na Jukwaa la Ushirikiano wa Afrika na China (FOCAC).

Mbali na hayo viongozi hao walijadili kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mshikamano wa nchi zinazoendelea, kudumisha amani na usalama, pamoja na kukuza mfumo wa kimataifa unaozingatia usawa na haki.

Ziara ya Wang Yi nchini inaendelea kudhihirisha dhamira ya Tanzania na China ya kuimarisha zaidi ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, ambapo kwa mwaka 2024 thamani ya biashara kati ya Tanzania na China ilifikia takriban dola za Marekani bilioni 5.2.

Kampuni za China pia zimeendelea kuwekeza nchini katika sekta za viwanda, kilimo, huduma, usafirishaji, mawasiliano na utalii.

Kwa mwaka 2025, Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ilisajili miradi ya China 343 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.1 na kuzalisha ajira 82,404.

Previous Post

MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

Next Post

RAIS DK. SAMIA AONYA WAVURUGA AMANI

Next Post
RAIS DK. SAMIA AONYA WAVURUGA AMANI

RAIS DK. SAMIA AONYA WAVURUGA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AZAM YAZITOLEA MACHO WYDAD, NAIROBI UTD NA AS MANIEMA

AZAM YAZITOLEA MACHO WYDAD, NAIROBI UTD NA AS MANIEMA

2 months ago

GAMONDI AJA KIVINGINE KUIVAA MOROCCO AFCON

6 days ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SABABU MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

    RAIS DK. SAMIA ATAJA SABABU MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DIAMOND KUTOKA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMANZI WATOTO WAKIFIA NDANI YA SWIMMING POOL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?