• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CCM INATEKELEZA AHADI KWA KASI – KIHONGOSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
CCM INATEKELEZA AHADI KWA KASI – KIHONGOSI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema utekelezaji wa ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilizoahidiwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu kupitia Ilani ya Uchaguzi, zinaendelea kutekelezwa kwa kasi kupitia kauli mbiu; Kazi na Utu, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi na Taifa.

Kihongosi aliyasema hayo, mkoani Singida katika Wilaya ya Manyoni, alipowasalimia mamia ya wannachi, waliojitokeza kumpokea kuanza ziara.

“Nawashukuru sana kwa mapokezi haya makubwa, nitoe salamu za Mwenyekiti wa Chama na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anajua niko hapa nimeanza ziara hapa Singida.

“Amenipa maneno yafuatayo, niwashukuru kwa kura za kishindo mlizompatia katika uchaguzi mkuu, anawapenda na kuwasaliamia sana.

“Pia, amenambia niwajulishe kuwa Kazi na Utu imeshaanza, kama alivyoahidi katika mikutano yake ya kampeni, kazi kubwa inaendelea kufanyika kwa lengo la kuchochea maendeleo kwa wananchi na Taifa,” alisema.

Aliwasisitiza wananchi wa Manyoni na Singida, kuendelea kudumisha amani na mshikamano wa kukijenga Chama na Taifa, kwani ndiyo msingi wa maendeleo na mafanikio.

Alieleza kuwa, Taifa liko imara kwa sababu ya uongozi thabiti wa CCM, unaoongozwa na Rais Samia.

Alisema ziara yake ilikuwa ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha nyingi zilizotolewa na Serikali ya Rais Samia, hivyo kuangalia kama miradi hiyo imekidhi kiwango cha fedha zilizotolewa.

Katika ziara hiyo, atatumia fursa ya kuzungumza na viongozi wa CCM kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo.

Aliwashukuru sana viongozi wa Mkoa wa Singida na wanachama kwa mapokezi makubwa waliyompa.

Katika hatua nyingine, Kihongosi, alitoa salamu za Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Asha – Rose Migiro, huku akiwaahidi kuwa kiongozi huyo atafika mkoani humo, kutembelea mashina na kuzungumza na wanachama.

Awali, akimkaribisha Kihongosi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, aliwapongeza mamia ya wanachama wa Manyoni kujitokeza kwa wingi kumkaribisha kiongozi huyo.

Mwenyekiti huyo, alisema mvua inanyesha, watu wanalima na chakula cha kutosha kipo mkoani humo, kwa sababu ya uchapakazi wa wananchi.

Previous Post

MWIGULU AKAZIA MAMBO NYETI

Next Post

KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

Next Post
KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

8 months ago
DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

5 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?