• ePaper
Tuesday, July 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WATU 120, 780 KUMCHAGUA MBUNGE JIMBO LA PERAMIHO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 26, 2026
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WATU 120, 780 KUMCHAGUA MBUNGE JIMBO LA PERAMIHO
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU, Ruvuma

WAPIGA Kura 127,632 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, watashiriki uchaguzi wa kuchagua mbunge wa Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma na Kata ya Shiwinga, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa, Jacobs Mwambegele, alisema hayo mjini Songea, akisoma risala kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakaofanyika leo ambapo vituo 373 vya kupigia kura, vitatumika.

“Kati yao, wapigakura 120,780 ni wa Jimbo la Peramiho na wapigakura 6,852 wapo katika Kata ya Shiwinga na jumla ya vituo 373 vya kupigia kura vitatumika.

“Vituo 354 vipo Jimbo la Peramiho, vituo 19 vipo Kata ya Shiwinga Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,”amesema Jaji Mwambegele.

Aidha, alisema kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Peramiho, vyama vya siasa 15, vimesimamisha wagombea na uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Shiwinga, vyama vya siasa vinane vimesimamisha wagombea.

“Natumia fursa hii kuvikumbusha vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi, kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumlishia kura.

“Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo na Kata husika, wamekamilisha utaratibu unaoweka mazingira yanayowawezesha mawakala wa vyama vya siasa, kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi,”alisema Jaji Mwambegele.

Alisema mawakala hao, wanawajibika kulinda maslahi ya vyama na wagombea wao, hivyo, wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni, utaratibu wa uchaguzi na maelekezo ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao vituoni.

“Vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi, kufungwa saa 10:00 jioni na ifikapo muda wa kufunga kituo saa 10:00 kamili jioni, kama wapigakura bado wapo katika mistari, mlinzi wa kituo, atasimama nyuma ya mtu wa mwisho na zoezi la upigaji kura litaendelea hadi wapigakura walio kwenye mstari watakapomalizika

“Baada ya kumaliza kupiga kura, mpigakura anatakiwa kuondoka eneo la kituo cha kupigia kura na mpigakura awapo kituoni, anatakiwa kufuata maelekezo yote atakayopewa na karani mwongozaji wapigakura,”alisema Jaji Mwambegele.

Jaji Mwambegele alisema mpiga kura ambaye ameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na taarifa zake zipo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililopo katika kituo husika, lakini amepoteza kadi au kadi yake imeharibika, ataruhusiwa kupiga kura kwa kutumia moja wapo ya vitambulisho cha Taifa NIDA, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria (passport).

Previous Post

SIMULIZI YA KUSIKITISHA ANAYEDAIWA KUUA MKE

Next Post

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

Next Post
YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA

CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA

5 months ago
VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

11 months ago

Popular News

  • CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WADAU WAMGOMEA SAMATTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?