• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 22, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

MAGWIJI wa soka nchini Boniface Pawasa na Mtemi Ramadhan wameyataka mabenchi ya ufundi ya Simba na Yanga kuhakikisha wanawasoma mapema wapinzani wao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya ugenini katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Yanga inatarajia kesho kucheza na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa hatua ya makundi utakaopigwa Uwanja wa Al Salam jijini Cairo huku Simba ikipepetana na Esperance de Tunis, utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Stade Olympique Mammadi nchini Tunisia, mechi zote zitapigwa kuanzia saa 1:00 jioni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakongwe hao walisema Simba na Yanga zina nafasi ya kufanya vyema katika mechi za ugenini kama  kila benchi la ufundi la timu hizo zitazingatia majukumu yao ipasavyo ikiwemo kuwasoma wapinzani.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Pawasa alisema Simba bado ina nafasi ya kufanya vyema katika mechi zilizobaki na kurudisha imani iliyotoweka kwa mashabiki.

Alisema benchi la ufundi la Simba linatakiwa kuwasoma wapinzani mapema na kutumia mbinu mbadala kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo na kurejesha imani kwa mashabiki wake.

“Benchi la ufundi la Simba linatakiwa kuhakikisha linawasoma wapinzani mapema na kujipanga kutumia mbinu mbadala ili kupata ushindi ugenini.

“Bado Simba ina nafasi ya kufanya vyema kwani hata misimu iliyopita tuliona timu ikipata ushindi ugenini na kufika mbali zaidi,” alisema Pawasa.

Pawasa alisema kitendo cha kuingia na kutoka ya makocha wa Simba imefanya kuishusha kiwango timu hiyo.

“Ndani ya kipindi kifupi Simba imefanya mabadiliko ya makocha kitu ambacho kinawachanganya wachezaji kwani kila mmoja amekuwa akija na falsafa zake,”alisema.

Alisema kila kocha aliyekuja Simba amekuwa na programu na falsafa zake hivyo kuwafanya wachezaji kushinda kutambua wafuate mbinu za nani wanapokuwa uwanjani.

“Kubadili makocha zaidi ya mmoja kwa kipindi kifupi, kimewachanganya wachezaji, hivyo uongozi unatakiwa kutumia mbinu mbadala kuirudisha timu hiyo katika mstari sahihi,” alisema Pawasa.

Kwa upande wake, kiungo wa zamani wa Simba, Mtemi alisema Simba bado ina kazi ya kufanya kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo unaofuata tofauti na Yanga.

Alisema Yanga ina timu nzuri na inaweza kwenda kutoa ushindani zaidi katika mchezo huo wa ugenini.

Alisema kwa Simba mechi inayofuata itakuwa ngumu kwani wakifungwa itakuwa wameondoa matumaini ya kusonga mbele tofauti na Yanga.

Mtemi aliongeza kwa upande wa Simba wanatakiwa kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanawakabili wapinzani wao na kupata ushindi.

“Timu ya Yanga ina nafasi nzuri kwani ina timu yenye wachezaji walio na muunganiko mzuri hivi sasa tofauti na Simba.

“Viongozi wa Simba wanatakiwa kujitathmini na kuangalia wapi walipokosea na kurekebisha mapema ili kuhakikisha wachezaji wanapambana na kupata ushindi katika mchezo huo,” alisema Mtemi.

Katika msimamo wa kundi D, Petro Atletico inaongoza kwa pointi nne sawa na Stade Malien zikitofautiana mabao ya kufunga, nafasi ya tatu inashikiliwa na Esperance de Tunis kwa pointi mbili huku Simba ikiburuza mkia bila pointi.

Kwa upande wa msimamo wa kundi B, Al Ahly ipo kileleni kwa pointi nne sawa na Yanga, zikitofautiana mabao ya kufunga, AS Far ipo nafasi ya tatu kwa pointi moja huku JS Kabylie ikiburuza mkia kwa alama yake moja.

Previous Post

AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

Next Post

RAIS DK. SAMIA KINARA UPANDAJI MITI

Next Post
RAIS DK. SAMIA KINARA UPANDAJI MITI

RAIS DK. SAMIA KINARA UPANDAJI MITI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI AITEKA RORYA | WANANCHI WATHIBITISHA KUTIKI OKTOBA  29 KWA KISHINDO

DK. NCHIMBI AITEKA RORYA | WANANCHI WATHIBITISHA KUTIKI OKTOBA  29 KWA KISHINDO

8 months ago
DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI

DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI

1 month ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?