• ePaper
Monday, May 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 26, 2026
in Makala, RIPOTI MAALUMU
0
SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA
0
SHARES
33
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

TATIZO la watoto kutelekezwa na baba kabla ya kulelewa na mama, linaendelea kuwa mfupa mgumu katika Jiji la Dar es Salaam.

Tafiti za taasisi za kimataifa zinaonesha mamilioni ya watoto barani Afrika, hukua bila uwepo wa baba katika kaya zao.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa data za Kidemokrafia na Afya (DHS), uliochapishwa mwaka 2017 na Umoja wa Mataifa (UN ), kati ya asilimia 30 hadi 40 ya watoto katika baadhi ya nchi za Afrika wanaishi na mama.

Changamoto hiyo inakinzana na usemi wa watoto ni zawadi kwa baadhi ya wanaume ambao huona mzigo na hatimaye kukwepa majukumu na kuishia kutelekeza familia.

Akizungumza na Uhuru, Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mwanamke na Mtoto, Nyamara Elisha, alisema suala la  wanawake kutelekezewa watoto na wenza wao ni changamoto kubwa ambapo takribani watoto 3,000 hadi 4,000 hutelelezwa kila mwaka katika mkoa huu.

Elisha alisema kundi kubwa la wanawake wanaofika kutoa taarifa ustawi wa jamii ni wale ambao hawajafunga ndoa.

“Suala la utelekezaji watoto lipo juu ni kati ya 3,000 hadi 4,000 kwa mwaka, kundi kubwa lipo kwa hawa wanaozaa pasipokuwa na ndoa,”alisema.

Alisema migogoro ya uhusiano, ndoa, ukosefu wa kipato, kutojiandaa kupata mtoto ni miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi ya wanaume kutelekeza wanawake waliozaa nao.

Alifafanua sababu nyingi za matukio hayo ni baba kukosa kipato na kutokuwa na uelewa wa sheria  ya ndoa kwamba baba ndiye ana wajibu wa kutunza familia.

“Suala la kipato limekuwa changamoto kubwa, baba anashindwa kutimiza wajibu anaona bora apotee au aondoke baada ya kuona kila hitaji anaombwa anaamua kutekeleza familia.

“Kutokuwa na maandalizi ya kuingia kwenye ndoa ni changamoto kubwa katika migogoro, mtu anapooa hatazami dhana kubwa ya ndoa kwamba anahitaji kuhudumia familia, mtoto anapoumwa atatakiwa kutoa fedha ya matibabu,”alisema.

Afisa Ustawi huyo alisema watoto wanaotelekezwa wanatendewa ukatili kwasababu hawapati mahitaji ya msingi kutoka kwa wazazi wake.

Aidha, alitaja sababu nyingine inayojitokeza mara kwa mara ni ukosefu wa mawasiliano baina ya wazazi wawili, ambapo baadaye huleta migogoro miongoni mwao.

Alisema kundi kubwa la wanawake vijana wenye wastani wa umri kuanzia miaka 20 hadi 35, ndiyo wanakwenda kutoa taarifa katika ofisi hizo kuhusu matukio ya utelekezaji watoto.

Hatua za Serikali

Aidha, Elisha alisema Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea kuchukua hatua mbalimbali, kupunguza utelekezaji.

Alisema miongoni mwa hatua hizo ni uanzishwaji wa Kamati za Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWA) ngazi za vijiji, kata na halmashauri.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Elisha alisema kamati hizo zina lengo la kusaidia malezi na makuzi ya watoto, huku zikishirikisha wataalamu na jamii.

Athari za Kisaikojia

Akizungumzia kadhia hiyo, Rais wa Chama Cha Wanasaikolojia Tanzania (TAPA) na Mhadhiri wa Saikolojia ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk. Magolanga Shagembe,alisema baba anapotelekeza familia huleta athari mbalimbali za kisaikolojia na kihisia kwa mtoto, zikiwemo huzuni ya kudumu, maumivu ya kihisia na hasira.

Dk. Shagembe alisema pia athari nyingine ni mtoto kujilaumu kwa kufikiri ndiyo chanzo cha baba kuondoka, kutojiamini katika maisha yake kwa kujiona hana thamani au hastahili kupendwa.

Daktari huyo alisema mtoto huweza kuwa na hasira ambayo anaielekeza kwa mzazi au kwa baadhi ya watu watakaomzunguka katika maisha ya baadaye kwa mume, mke, wafanyakazi wenzake na  watoto wake.

Vilevile Dk. Shagembe alisema athari nyingine mtoto akiwa mkubwa hukwepa kumwamini mtu, uasi, ukaidi na kujitenga.

Mtaalamu huyo anaongeza mzazi anayetelekezewa watoto husongwa na majukumu, msongo wa mawazo, kiuchumi, uchovu wa kihisia na kuathiri upatikanaji wa huduma muhimu.

Aidha, Dk. Shagembe alisema baadhi ya watoto hushuka viwango vya masomo darasani na kupoteza umakini.

Kwa upande wake, mtaalamu wa afya ya akili Dk. Pascal Kang’iria, alisema mtoto anapaswa kulelewa na wazazi wawili kuanzia umri wa 0 hadi miaka 17.

Mtaalamu huyo alisema mtoto anapolelewa na mzazi mmoja pekee hushindwa kujifunza kutoka kwa wazazi wote wawili.

“Baba akiwepo na mama mnatengeneza mtoto bora na thabiti katika ukuaji wake, kwa kuwa mama bora au baba bora anayeweza kukabiliana na mambo mbalimbali ukubwani,”aliongeza.

Kauli ya Dk. Gwajima

Januari 23, mwaka huu, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dk. Dorothy Gwajima, aliitaka Sekretarieti ya Uratibu wa Mpango wa Kitaifa wa Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II) kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha vitendo hivyo vinapungua nchini.

Dk. Gwajima alisema hayo Dodoma katika kikao cha waratibu wa MTAKUWWA II kilichofanyika kwa njia ya mtandao kwa kushirikisha viongozi wa wizara na maofisa maendeleo na maofisa ustawi wa jamii wa mikoa.

Alieleza wizara imeendelea kushirikiana na wizara za kisekta na wadau wa maendeleo kuratibu MTAKUWWA II 2024/2025 – 2028/2029), ambao una maeneo manane ya utekelezaji, yakiwemo kuimarisha uchumi wa kaya, mila na desturi.

Pia, mazingira salama katika maeneo ya umma na mtandaoni, malezi, msaada wa familia na uhusiano, utekelezaji na usimamizi wa sheria na utoaji wa huduma kwa wahanga na manusura wa ukatili.

Waziri huyo alisema ili kupambana na ukatili wa aina zote, lazima Waratibu wa Mpango huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika ngazi ya mikoa, wilaya, kata na mitaa kupata kuelewa dhana na majukumu ya Kamati za MTAKUWWA ngazi za kata na vijiji na mitaa.

“Ninawaomba wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA na sekretariati yake kuimarisha mifumo ya mawasiliano na utoaji wa taarifa kwa umma, njia hii itatoa namna ya kuendelea kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kushirikishana mafanikio yanayopatikana katika utekelezaji,” alisema Dk. Gwajima. 

Previous Post

MFALME WA MOROCCO ATOA NENO AFCON

Next Post

BODABODA, MACHINGA, MAMA LISHE SHANGWE

Next Post
BODABODA, MACHINGA, MAMA LISHE SHANGWE

BODABODA, MACHINGA, MAMA LISHE SHANGWE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

1 month ago
KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

2 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KILIO CHA BANDO CHATUA BUNGENI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA KIHONGOSI YAACHA NEEMA KWA WANAWAKE MARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAJIPANGA KUDHIBITI MIJI HOLELA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?