• ePaper
Friday, April 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MFALME WA MOROCCO ATOA NENO AFCON

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 24, 2026
in Burudani, Michezo
0
MFALME WA MOROCCO ATOA NENO AFCON

Mohammed VI

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RABAT, Morocco

MFALME wa Morocco, Mohammed VI amesema undugu wa Afrika kupitia michezo utaendelea japokuwa taswira yake ilichafuliwa na baadhi ya matukio yaliyotokea wakati wa fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), zilizofanyika nchini Morocco.

Fainali hizo zilimalizika Januari 18, mwaka huu kwa kuzikutanisha Morocco dhidi ya Senegel ambapo wenyeji walipoteza bao 1-0.

Alisema kuna baadhi ya matukio ambayo yaliichafua taswira ya michuano ikiwemo kundi la mashabiki kuvamia walinzi waliokuwa uwanjani.

Alisema kwa muda mrefu, Senegal imekuwa moja ya washirika wa karibu wa Morocco barani Afrika, ambapo makampuni na benki za Morocco zimepanua uwekezaji katika miaka ya hivi karibuni na kuimarisha masuala la kidiplomasia katika ufalme huo.

Alisema saa chache baada ya kumalizika fainali hizo, mitandao ya kijamii katika nchi hizo ilikuwa katika hali ya mvutano kitu ambacho hakikuwa kizuri.

“Fainali iligubikwa na matukio mbalimbali ambayo mengine yalionekana wazi, hii siyo tabia nzuri.

“Japokuwa fainali zilikuwa na mambo mengi, undugu wa Afrika kupitia michezo utaendelea kuwepo.

“Hakuna kitu kinachoweza kudhoofisha uhusiano wa karibu ulioanzishwa kwa karne nyingi kati ya watu wetu wa Kiafrika, wala ushirikiano wenye manufaa uliojengwa na nchi katika bara zima na kuimarishwa kwa ushirikiano uliopo.

“Mashindano hayo pia yalionyesha maendeleo na mafanikio ya Morocco kupitia mchezo wa soka,” alisema.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limesema linaendelea na uchunguzi wa matukio yote yaliyotokea katika mchezo wa fainali huku Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),  Gianni Infantino akilaani tabia za wachezaji na benchi la ufundi la Senegal.

(Livescore)

Previous Post

ESPERANCE, SIMBA MECHI YA HESABU

Next Post

SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

Next Post
SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

2 weeks ago
DK. SAMIA AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM

DK. SAMIA AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM

6 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AWASHUKIA WACHOCHEZI MIGOGORO

    WAZIRI MKUU AWASHUKIA WACHOCHEZI MIGOGORO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKWELI HADHARANI TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YASIJIRUDIE TENA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MSD YABAINISHA DHAMIRA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA YA AFYA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?