• ePaper
Friday, May 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 22, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano wa kuigwa duniani katika upatikanaji wa maji safi na salama.

Dk. Nchimbi amesema hayo mkoani Morogoro, katika Kilele cha Wiki ya Maji mwaka 2026.

Amesema japokuwa upatikanaji wa maji yasiyo salama bado ni changamoto kubwa duniani, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu.

“Sera ya maji ya mwaka 2002, Toleo la 2025 inasisitiza upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watanzania wote, kutokana na kufuata vizuri na kutekeleza sera hii katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuwafikishia watu maji safi na salama,”amesema.

Amesema hivi sasa zaidi ya asilimia 82.5 ya Watanzania waliopo vijijini na zaidi ya asilimia 92.5 waishio mijini, wanapata huduma za maji safi na salama.

Amebainisha tayari vijiji 10,758 vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama, huku vijiji 1,575 vikiwa bado havijafikiwa.

“Kipekee tunampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Maji na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimamia sera zake.

“Ninafurahi kuona watendaji wa Wizara ya Maji wanaimba 1,575 inatia moyo na katika hotuba ya Rais Dk. Samia katika ufunguzi wa Bunge mwaka 2021, alitaja ajenda yake kubwa ni kumtua mama ndoo kichwani na ajenda hii itafanikiwa ikiwa kutakuwa na miradi itakayofanyika kwa haraka na ufanisi,” amesema.

“Ndiyo maana Rais Dk. Samia aliwaweka aina ya watu katika Wizara ya Maji ambao wanaakisi matarajio yake na hao wameonesha kwa vitendo, ninaipongeza Wizara ya Maji kwa kazi nzuri mnayoifanya,”amesema.

Balozi Dk. Nchimbi amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inazungumzia maendeleo makubwa ikiwemo kuinua kipato cha Watanzania kufikia ngazi ya kati, juu katika miaka michache inayokuja ndani ya dira hiyo.

“Tunapofurahia habari za kuendeleza vyanzo vyetu vya maji lazima tuangalie umuhimu wa kulinda maji, tufanye uwekezaji wa kimkakati kama ambavyo sera yetu inavyotuambia tufanye uwekezaji unaoangalia umuhimu wa vyanzo vya maji kuvilinda na kuvitunza.

Amesema wakati inapotekelezwa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, lazima mkazo uwekwe katika Gridi ya Maji ya Taifa kwa kuwa ni tamaa ya kila Mtanzania kuona mpango huo unafanikiwa na kuondokana na changamoto ya maji.

Dk. Nchimbi amesema ni muhimu kubuni vyanzo vipya vya mapato katika kukuza sekta hiyo, badala ya kutegemea chanzo cha aina moja.

“Tuwe na vyanzo vingi mbadala ambapo Mamlaka ya Maji Tanga imetoa mfano wa kuigwa, imetuonesha unaweza kuanzisha mchakato wa bodi ya maji, kitu ambacho wamekifanya tujifunze kupitia wao,” ameeleza.

Hata hivyo, Makamu wa Rais Dk. Nchimbi ametahadharisha akitaka uwepo mpango kuepusha maji taka kuingiliana na maji safi na salama.

WAZIRI WA MAJI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alimshukuru Rais Dk. Samia kutokana na kuwatoa mbali katika wizara hiyo.

“Rais Dk. Samia ametutoa mbali, wizara yetu ya maji itoshe kusema Dk. Samia ni suluhu ya matatizo ya Watanzania maelekezo yake anataka matokeo.

“Makamu wa Rais umeendelea kusisitiza unataka matokeo na Waziri Mkuu pia anataka matokeo, hivyo napenda kuwahakikishia hatutakuwa kikwazo kwa Watanzania kupata huduma za maji,”alisema Aweso.

MUSSA AZZAN ZUNGU  

Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, alisema aliwahi kuwa diwani katika Manispaa ya Ilala mwaka 2000, ambapo mradi wa Kidunda uliletwa na MCC na ukajengwa mwaka 2001.

“Mradi ule ulipotea hewani haukujengwa hadi alipokuja Rais Dk. Samia na kuamua kuujenga.

“Ninamshukuru Rais Dk. Samia kwa ujasiri na hatua ya kuamua kujenga Mto Ruvu, unapoteza lita milioni 600 za maji ambayo yanapotelea baharini, kwa sababu hakuna sehemu ya kuhifadhia maji hayo,” alisema.

PROFESA KABUDI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalumu), Profesa Palamagamba Kabudi, alisema Mkoa wa Morogoro una umuhimu mkubwa katika sekta ya maji.

“Mkoa wa Morogoro pekee yake una vyanzo 177 vya maji kwa shughuli za kilimo, umeme na watu wengi hawaelewi Morogoro una mabwawa matatu makubwa ya maji ikiwemo Udzungwa, Kidatu na Bwawa la Mwalimu Nyerere zaidi ya asilimia 65 ya bwawa hilo lipo Morogoro na sehemu kubwa ipo Kilombero na inayofuata Liwale halafu Mkoa wa Pwani.

“Pia, inatoa megwati 2,115 ambapo Kihansi megawati 180, Kidatu megawati 204 na kidatu ilijengwa kwa sababu ya viwanda vikubwa vya chuma kwa kutoa chuma kutoka Mchuchuma na kuleta Kidatu au kupeleka Makambako, vitumie reli ya kati,” alisema.

Profesa Kabudi alisema unahitajika mpango kabambe wa maji kwa mkoa huo wenye milima ya Uruguru, Rubeo, Mahenge, Udzungwa na Ukaguru.

MKUU WA MKOA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, alisema wakazi wa mkoa huo wanamshukuru Rais Dk. Samia kwa ahadi ya kupambana na mafuriko ambayo anataka yafike mwisho.

“Tuna ahadi ya kupokea mabwawa ya kuvuna maji ambayo yatatumika kwa huduma za maji na umwagiliaji katika shughuli za kilimo.

Alisema hivi sasa wataalamu wa Bonde la Wami Ruvu, wanafanyia kazi mfumo wa mafuriko hayo, kubaini maeneo ambayo yanatakiwa mabwawa ya kuvuna maji yakae.

“Tuna imani kwa upande wa Kilosa, Mvomero, Kilombero yatapunguza mafuriko ambayo tunakumbana nayo. Tuna matarajio kadhia hii ya mafuriko kila ifikapo Februari, Machi na Aprili, hali hii inatarajiwa kuondoka, tunaomba umfikishie salamu zetu za pongezi Rais Samia,” alisema.

Alisema katika mkoa huo kuna miradi ya maji yenye thamani zaidi ya sh. bilioni 400, huku inayotekelezwa vijijini pekee ikiwa na thamani ya sh. bilioni 120.

KATIBU MKUU

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri alisema walianza kuadhimisha siku ya maji Machi 16, mwaka huu kwa kufanya shughuli zinazohusu sekta ya maji.

Previous Post

SERIKALI YAIFANYA MWANZA KITOVU KIKUU CHA KIUCHUMI

Next Post

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

Next Post
MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

5 months ago
KIWANGO SIMBA CHAMKERA BARKER

KIWANGO SIMBA CHAMKERA BARKER

4 months ago

Popular News

  • MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    MWANZO, MWISHO SIMULIZI MAUAJI YA MCHINA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?