• ePaper
Sunday, March 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

TRA YAJIVUNIA MAFANIKIO NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 3, 2026
in Makala
0
TRA YAJIVUNIA MAFANIKIO NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS DK. SAMIA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na JOE NAKAJUMO

WIZARA ya Fedha ndiyo moyo wa serikali kwa maendeleo ya nchi. Ni kauli ya Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar.

Waziri alitoa kauli hiyo katika mkutano wake na wafanyakazi wa wizara baada ya kuapishwa kuongoza Wizara ya Fedha.

Aliwakumbusha kuwa wizara hiyo, imebeba matumaini ya serikali na wananchi, katika kuhakikisha inatafuta fedha za kuendeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo, itakayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi.

Kwa mantiki hiyo, Waziri anaitaka menejimenti na wafanyakazi wote, kujipanga kikamilifu kuhakikisha fedha zinapatikana. Wizara inatakiwa kuweka mikakati na mipango madhubuti ya kutafuta raslimali za ndani, kuendeleza na kukamilisha miradi mbalimbali.

Balozi Omar, anawaambia wafanyakazi wa wizara kwamba wana jukumu kuweka sera bora za fedha, zitakazo saidia kuyawezesha makundi mbalimbali wakiwemo vijana kupata ajira na kufanyabiashara.

Pia, kuyasikiliza makundi mbalimbali yenye changamoto zinazokwamisha ustawi wao,wakati nchi ikianza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Miongoni mwa taasisi za umma, zenye jukumu la kutafuta fedha za kuendesha nchini Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA). Hii ndiyo yenye kazi ya kukusanya kodi, sehemu kubwa ikiwa kutoka kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.

TRA, ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 11 ya mwaka 1995 na ilianza kufanya kazi Julai Mosi, mwaka 1996.

Kauli mbiu yake ni ‘PamojaTunajengaTaifaLetu’. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa na mafanikio mwaka hadi mwaka katika majukumu yake ya kukusanya kodi.

TRA YAVUNJA REKODI

Mfano mzuri ni Disemba mwaka jana, TRA ilivuka lengo la makusanyo. Kamishna Mkuu waTRA,Yusuph Mwenda, alisema Desemba mwaka jana walivuka lengo kwa kukusanya trilioni 4.130,wakati lengo lililowekwa kwa mwezi huo lilikuwa likikukusanya sh. trilioni4.14.

Makusanyo hayo makubwa ya kuvuka lengo yalifanywa ndani ya siku 100 za kwanza za muhula wa pili wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kuonyesha dhahiri jinsi TRA ilivyojipanga vizuri katika ukusanyaji mapato.

“Kiasi hiki ni kikubwa mara ya kwanza hakijawahi kukusanywa na TRA kwa mwezi mmoja.  Disemba mwaka 2024, tulikusanya sh. trilioni tatu na bilioni 500,”alieleza Kamishna Mkuu Mwenda.

Takwimu za makusanyo, zinaonyesha kwa miezi mitatu, kuanzia Oktoba hadi Disemba,mwaka jana 2025,TRA ilikusanya sh. trilioni 9.8. Kamishna Mwenda alisema wastani wa ukusanyaji kodi kwa mwezi, umepanda kutoka sh. trilioni 2.7 hadi sh. trilioni 3.130.

TRA imekusanyash.trilioni 18.7 kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha wa 2025/2026, ikivuka lengo la kukusanya sh. trilioni 18.1.Lengo la makusanyo kwa mwaka huu wa fedha ambao ulianza Julai Mosi, mwaka jana 2025 na kumalizika Juni 30, mwaka huu wa 2026 ni sh. trilioni 36.

SABABU ZA MAFANIKIO

Kamishna Mkuu Mwenda alizitaja sababu za mafanikio katika ukusanyaji kodi kuwa ni kutokana na uhimilivu wa uchumi uliopo nchini ,sera za uchumi, ulipaji kodi kwa hiari na mfumo mzuri wa kodi uliowekwa na jitihada za utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa TRA.

Mwaka huu, alisema Kamishna Mkuu Mwenda, kwamba TRA imejipanga kusimamia sheria za kodi, kupambana na wakwepa kodi na kuendelea kusimamia uadilifu kwa watendaji wa Mamlaka.

MFUMO MTANDAO

TRA itaboresha huduma zake kwa kuanzisha mfumo mpya wa kodi za ndani, uliopangwa kuanza Januari mwa kahuu. Kupitia mfumo huo, mambo mengi yatafanyika kwa mtandao ‘online’. Hii itapunguza usumbufu kwa walipa kodi kwenda ofisi za TRA.

Mwenda alisema mfumo mpya utafanywa kidijitali,  hatua ambayo itarahisisha utendaji kazi, kuboresha huduma kwa walipa kodi na kuondoa malalamiko.

 Alisema kupitia mfumo, makadirio ya kodi yatakayo toka baada ya matumizi ya mfumo yatakuwa sahihi na utatoa haki kwa walipa kodi.

SHUKRANI KWA RAIS SAMIA

Kuhusu mafanikio ya TRA, Kamishna Mkuu Mwenda, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kujenga uchumi himilivu na kwamba mfumo mpya unatimiza maono ya Rais, kutaka mifumo ya serikali isomane.

Akifafanua matumizi ya mfumo mpya wa ulipaji kodi, Kamishna wa Kodi za Ndani, Alfred Mregi, aliutaja kuwa ni Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani na lengo ni kuondoa changamoto kwa wafanyabiashara na walipa kodi katika ulipaji kodi.

TAASISI 300

Kamishna Mregi alisema mfumo una uwezo kuunganisha zaidi ya taasisi 300 na unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 9, mwaka huu.

“Tumelenga kuunganisha mfumo katika taasisi 300,kwa kuanzia tunaanza na 60 ziendelee kutoa huduma ya kuwasiliana moja kwa moja bila mfanyabiashara au mlipa kodi kufika ofisi zetu,”alifahamisha Mregi.

Aliwashauri wafanyabiashara kutumia mfumo huu mpya kwa kuwa una manufaa kwa pande zote mbili, kulipa kodi kwa stahiki bila malalamiko na serikali inapata mapato.

ELIMU YA FEDHA

Katika hatua nyingine, serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau imeandaa nyenzo za kufundishia elimu ya fedha . Inajumuisha mada zinazohusu usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji wa akiba, mikopo ,uwekezaji, bima, bima ya amana, kodi na hatifungani.

Serikali inalenga ifikapo mwaka 2030, asilimia 80 ya Watanzania wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha. Utafiti wa Fin Scope, uliofanyika mwaka 2023, uligundua  ni asilimia 53.5 ya nguvu kazi nchi ni iliyotumia huduma rasmi za fedha.

Hali hii inaonyesha umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuongeza ushiriki wa wananchi katika mifumo rasmi ya fedha.

Previous Post

WIZARA YA VIWANDA YAZALISHA AJIRA LUKUKI NDANI YA SIKU 100

Next Post

TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

Next Post
TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

EDNA LEMA AWAITA MASHABIKI KMC

EDNA LEMA AWAITA MASHABIKI KMC

2 months ago
CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

5 months ago

Popular News

  • SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FCC, TCRA KUCHUNGUZA GHARAMA ZA BANDO NCHINI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?