• ePaper
Friday, April 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 6, 2026
in Burudani, Michezo
0
ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

KATIKA kuendelea maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika  (AFCON 2027), Kamati ya Kitaifa ya mashindano hayo, imeanza kuweka mikakati madhubuti ya ulinzi na usalama michezoni.

Hayo yalielezwa katika kikao cha kamati hiyo kilipokutana na Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Michezo kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Valeroo de Divitiis, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Boniface Tamba alisisitiza umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya ulinzi na usalama itakayohakikisha mashindano ya AFCON 2027 yanafanyika katika mazingira salama.

Alisisitiza michuano hiyo ambayo itashirikisha mataifa mbalimbali ya Afrika, inatakiwa kufanyika katika hali ya utulivu na inayokidhi viwango vya kimataifa.

Alibainisha kuwa Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi waandaji, ina wajibu wa kuhakikisha miundombinu ya viwanja, mifumo ya udhibiti wa umati, na usimamizi wa matukio makubwa ya michezo vinaimarishwa kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.

Alisema kikao hicho kililenga kuimarisha uratibu kati ya taasisi za usalama na michezo, kufanya tathmini ya vihatarishi (risk assessment) na kuweka mifumo thabiti ya usimamizi wa usalama itakayohakikisha Tanzania inatimiza wajibu wake kama mmoja wa waandaji wa mashindano hayo makubwa barani Afrika.

“Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi waandaji, ina wajibu wa kuhakikisha miundombinu ya viwanja, mifumo ya udhibiti wa umati na usimamizi wa matukio makubwa ya michezo vinaimarishwa kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa,” alisema.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON 2027, Leodegar Tenga alisema dhamira ya serikali na wadau wa michezo ni kuhakikisha mashindano ya AFCON 2027 yanafanyika kwa mafanikio makubwa.

Alifafanua mafanikio hayo ni nje ya ubora wa kiufundi wa michezo, bali kwa viwango vya juu vya ulinzi na usalama.

Msimu ujao wa fainali za michuano ya AFCON 2027, zinatarajiwa kufanyikia katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Previous Post

MAKATIBU WAKUU VYAMA VYA UKOMBOZI WAJADILI HALI YA KISIASA KUSINI MWA AFRIKA

Next Post

RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

Next Post
RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WANADIPLOMASIA WATAJA FAIDA TANO ZA AMANI NCHINI

WANADIPLOMASIA WATAJA FAIDA TANO ZA AMANI NCHINI

3 months ago
AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

7 months ago

Popular News

  • KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • LAZARUS CHAKWERA AMALIZA ZIARA YA SIKIU 9 NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?