• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

RAIS DK. SAMIA AIJAZA MAMILIONI TWIGA STARS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 3, 2025
in Burudani, Michezo
0
RAIS DK. SAMIA AIJAZA MAMILIONI TWIGA STARS
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi ya sh. milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026), zitakazofanyikia nchini Morocco.

Twiga Stars ilifuzu michuano hiyo baada ya kuichapa Ethiopia kwa mabao 3-0, ikishinda 2-0 nyumbani na kuitandika 1-0 ugenini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, alisema Rais Dk. Samia ametoa fedha hizo ikiwa ni hamasa kwa Twiga Stars.

Alisema wamepewa fedha hizo kuhakikisha wanajipanga vyema kwenda kushiriki katika fainali za WAFCON 2026 zitakazofanyika Machi, mwakani nchini Morocco.

Alisisitiza Rais Dk. Samia anawapongeza Twiga Stars kwa kufuzu kucheza fainali hizo msimu ujao.

“Rais Dk. Samia ametoa kiasi cha sh. milioni 50 kwa Twiga Stars kutokana na kufuzu kucheza fainali za WAFCON 2026.

“Amewapongeza na ametuelekeza kuhakikisha timu haishuki kiwango na itaendelea kufanya vizuri zaidi katika michuano mbalimbali itakayoshiriki,” alisema Msigwa.

Alisema serikali itaendelea kutoa sapoti kwa timu hiyo na kuendeleza mpango wake wa kutumia michezo kimkakati ikiwemo kuvutia watalii na wachezaji kupata ajira nje ya nchi.

Previous Post

TUMEJIPANGA

Next Post

MKWASA, MTEMI WACHOMBEZA TAIFA STARS

Next Post
MKWASA, MTEMI WACHOMBEZA TAIFA STARS

MKWASA, MTEMI WACHOMBEZA TAIFA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO KWA MA -RC

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO KWA MA -RC

5 months ago
SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI IKULU ZANZIBAR

SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI IKULU ZANZIBAR

4 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?