• ePaper
Wednesday, May 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa ameongoza kusanyiko la wajumbe wa Taasisi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera, (KADEFO) huku akitaja jitihada za serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuufungua kimaendeleo Mkoa wa Kagera kupitia uendelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati.

Pia, amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADEFO, Balozi Liberata Mulamula, viongozi wengine na wanachama wa jumuiko hilo kwa kuimarisha taasisi hiyo na kudumisha umoja kwa wananchi kwa lengo la kuchochea maendeleo ya mkoa huo huku akisisitiza uwajibikaji katika utekekelezaji wa mikakati yao ili kufikia malengo.

Balozi Dk. Kakurwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na  wajumbe wa KADEFO, iliyowakutanisha Wanakagera kwa lengo la kujadili na kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo.

Ametaja mikakati hiyo ya serikali ya kuendeleza mkoa huo ni ujenzi wa tawi la Chuo kikuu cha Dar es Salaam,(UDSM) fursa za ufugaji kupitia uwekezaji wa ranchi, kuimarisha upatikanaji chakula, uvuvi wa kisasa, kilimo na kuimarisha viwanda vya usindikaji, kuunganisha katika gridi ya Taifa ya umeme.

Awali akifungua jumuiko hilo la KADEFO, Mwenyekiti wa  Bodi ya Wakurugenzi ya taasisi hiyo, Balozi Liberata Mulamula, alitaja lengo la taasisi hiyo ni kudumisha umoja na kuweka mikakati ya kuendeleza mkoa huo kiuchumi kwa kuvutia wawekezaji kwa fursa zilizopo.

Alitaja baadhi ya manufaa yaliyopatina katika taasisi hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia IT, kwa vijana wa mkoa huo, kuwaunganisha wanakagera, na kufanikisha majumuiko mbalimbali ya KADEFO na kuandaa mradi wenye thamani ya sh.milioni 300 utakao anza kwa michango ya wajumbe.

Alimshukuru mgeni rasmi, Balozi Dk. Bashiru kwa kukubali mwaliko huo, jambo ambalo limewapa heshima kubwa huku akiwashukuru wajumbe wote waliojitokeza na kutoa maoni yao mbalimbali katika kuendeleza mkoa huo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Nazir Karamagi, alisema mkoa huo unazofursa nyingi za uwekezaji ni wakati muafaka wa wanakagera wenyewe kuwekeza kuvutia wengine, hali itakayosaidia kuinua uchumi huku akipongeza uongozi wa KADEFO, kwa jitihada kubwa za kuwakutanisha wanakagera wote, na pendekezo zuri la mradi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahaya Kido, aliwapongeza wajumbe wa taasisi hiyo walioudhuria jumuiko hilo, huku akipongeza dhamira na jitihada zao za kukwamua mkoa huo na kuweka wazi utayari wake wa kushirikiana na wananchi wa mkoa huo kuchochea maendeleo.

Akiwasilisha salamu za wabunge wengine, Katibu wa Wabunge wa Mkoa huo, Florent Kyombo,ambaye ni mbunge wa Misenyi alisema wote wamefurahishwa na kufanyika kusanyiko hilo na walishiriki katika maandalizi.

Previous Post

TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

Next Post

IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

Next Post
IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA APOKEA UJUMBE WA RAIS PUTIN

RAIS DK. SAMIA APOKEA UJUMBE WA RAIS PUTIN

6 months ago
KASI YA DK. MWIGULU YAWAIBUA WASOMI

KASI YA DK. MWIGULU YAWAIBUA WASOMI

6 months ago

Popular News

  • BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?