• ePaper
Monday, May 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ameahidi kuwashughulikia watu wote wanaotumia mabavu kupoka haki za watu.

Dk. Mwigulu, alisema hayo mkoani Iringa, alipokagua ujenzi wa barabara ya lami Ipogolo – Kilolo yenye urefu wa kilometa 33.61.

“Unakuta mahakama ishaelekeza mwenye haki ni mtu fulani, yule ambaye amepora haki, anang’ang’ania kwa nguvu.

“Serikali inaingilia kati kunusuru, yule ambaye anataka kutumia mabavu ya kupora haki ya mtu.

“Na mimi kote nilipotoka na sehemu zingine ambazo bado sijapita, ninaendelea kuwaambia kuwa, kama unajua umetumia mabavu na hiyo haki haustahili, mapema umrejeshee anayestahili,”alisema.   

Waziri Mkuu, alisema atakuwa anapata taarifa za kila mkoa kwa kila mwezi na kwa wale ambao hawatafanya hivyo kwa hiyari yao, atawashughulikia wote ambao wanawakosesha haki wenzao.

“Hakuna mahali panaposema mtu akishakuwa na mali, tajiri wewe ni Mtanzania na nusu na wengine ni nusu ya Watanzania, kwa hiyo tuyazingatie hayo,”alisema.

Alisema amepita baadhi ya maeneo, amekuta kuna ujasiri wa watu kukanyaga haki za watu kwa kiwango cha juu.

“Watu wanajua sheria ya fidia inasemaje, pia wanatambua umuhimu wa miradi ya maendeleo wanakwenda katika eneo la mtu, wanasema tunataka kujenga shule wanalichukua hawafanyi malipo ya fidia,” alisema.

Mwigulu alisema wapo wengine wanaotumia jina la Rais Samia vibaya wakidai kuwa, ardhi yote ni mali yake.

“Nendeni mkaisome vizuri sheria, si tuna wanasheria hadi wilaya, mikoa someni vizuri, Rais anashikilia ardhi kwa niaba ya Watanzania, ninyi huku mnanukuu bila kuona naye.

“Nimesikia ana kwa ana akituelekeza wasaidizi wake pamoja na kuwa, tunataka uwekezaji na maendeleo, msipore ardhi ya wananchi bila ya kuwalipa fidia, ninyi mmetoa wapi maelekezo mengine,”alisema.

Alieleza kuna sehemu zingine wala siyo uwekezaji, mtu anakwenda kuchukua eneo la mtu kwa kuwatumia watu wa ardhi, akamchukulie eneo kwa kuwaelekeza waseme kuna mwekezaji.

ASIKILIZA KERO YA UPORWAJI WA HAKI

Katika mkutano huo, alisikiliza kero mbalimbali, ikiwemo uporwaji wa haki ambapo mkazi wa mkoa huo, Betty Mgohole, alisema kaka yake alimiliki eneo tangu mwaka 1982 lililopo Kimbizi na ilipofika mwaka 1998, akaanza kuumwa, halmashauri ilipima eneo hilo na kumpa mwekezaji.

“Kaka yangu alifariki na kuacha watoto wawili, mimi nilikuwa ndiyo msimamizi wa mirathi, kati ya watoto hao, mmoja aliachwa akiwa na umri wa miaka 13 na akawa analelewa na bibi yao.

“Wakaona mawe yanamwaga ndiyo wakanipigia simu, tukaenda na watoto hadi eneo la tukio, tukawauliza majirani wakasema tunaona watu wanakuja hapa, tukajua ninyi mmeuza, tukawaambia hatuwezi kuuza wakati watoto wa marehemu wapo,”alisema.

Alisema waliwatafuta hao watu, wakawapata, wakadai wamepimiwa na halmashauri na fidia walitoa halmashauri.

“Wakasema basi naomba tuelewane, nikawaambia sina mamlaka,  sababu eneo hilo ni la watoto, wakasema tushalipa halmashauri na eneo ni la kwetu, nikaenda mahakamani nikafungua mashataka nikashinda kesi,” alisema,

Alisema baadaye walikata rufani kwenda Mahakama Kuu, wakashinda kesi walipokuwa wanafuatilia gharama za uendeshaji wa hiyo kesi, akaambiwa kuwa, mdogo wake ameitwa mahakama ya wilaya wakamfanyie uhakiki sahihi.

“Mara nikaona wakili wa mwekezaji akaja akasema  tumeiona barua kuwa, eneo lile ni la mdogo wake marehemu, siyo marehemu mwenyewe, wakafungua kesi nyingine kwa jina lingine, watu ni wale wale,”alisema

Alisema katika kesi hiyo, hakimu ambaye alimpatia ushindi katika kesi ya awali, akampatia ushindi mwekezaji.

Betty alisema wakati kesi inaendelea, halmashauri ilikuwa inafanya mchakato wa kumtengenezea hati apate haki.

“Hakimu akaniambia haki itakuwa kwa huyu mwekezaji kwa sababu, ana hati na barua tumeikamata lile eneo siyo la marehemu, akaitwa mdogo wa marehemu, akaja mahakamani akaulizwa akasema eneo lile siyo la kwake bali ni la marehemu,”alisema.

Baada ya kusikia malalamiko hayo, Waziri Mkuu Dk. Mwigulu, alielekeza kusitishwa kwa utoaji wa hati ambayo inataka kutolewa kitapeli, kwa mtindo wa unyang’anyi.

“Mpaka tujiridhishe na utaratibu wa kisheria ulivyoelekezwa hapa, haya mambo ya kitapeli ebu Mkuu wa mkoa mtume RPC wakamatwe hawa watu ambao wanafanya fujo za kijinga, wawekwe ndani.

“Mambo ya kuwaonea watu bila sababu, RPC kamata hao weka ndani tafuta wanasheria, tunatafuta matapeli kila siku, fungua kesi matapeli ya aina hii, michezo ya kufanya njama kudhulumu watu, RPC wasakwe hao wafungulieni mambo ya kitapeli,” alisema

Waziri Mkuu huyo, alisema watu wa aina hiyo, ndiyo anaowatafuta kuwashikisha adabu na kwamba, wakamatwe wawekwe ndani wafunguliwe mashitaka ya utapeli.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu aliwataka watendaji wa serikali waache kufanya ubosi katika kazi za watu na waziheshimu kazi zao.

Alitoa wito huo juzi, alipozungumza na wakazi wa Iringa mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kichangani, Kihesa, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.

 “Lazima tuheshimu kazi za watu, tuheshimu jitihada za kila mmoja na tusifanye ubosi kwenye kazi za watu,”alisema.

Dk. Mwigulu alimwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, awape maelekezo watumishi waliopo katika halmashauri zote za mkoa huo na kuwataka waache kukamata vitendea kazi vya wananchi.

“Mkuu wa Mkoa, watangazie viongozi wa halmashauri zote za mkoa wako, wasikamate vitendea kazi vya wananchi. Sitaki kusikia sahani wala bakuli ya mamalishe imekamatwa.

“Endapo vitendea kazi hivyo vimehusika na kazi za uhalifu kama ujambazi, ubakaji, dawa za kulevya au meno ya tembo, ndipo vinaweza kuchukuliwa kama vidhibiti, kwani hayo ni makosa ya jinai,”alisema.

Wakati huo huo, Dk. Mwigulu alifanikisha kurejeshwa sh. 600,000 kwa Gideon Yona, ambazo zilikuwa za mtaji wa biashara yake ya dagaa.

Akielezea kero yake mbele ya Waziri Mkuu, Yona alisema kuwa, Februari 26, mwaka huu, alipofika Soko la Mlandege, Iringa alikuta magunia yake ya dagaa yameibwa, aliripoti kwa mwenyekiti wa soko, hadi leo hajarudishiwa dagaa wala fedha yoyote.

Alipoulizwa kama analifahamu suala hilo, Mwenyekiti wa soko hilo, Kessy Michael Ndandu, alikiri kulitambua na kwamba, siku ya tukio, alitoa taarifa kwa Ofisa Biashara wa Manispaa, Mahenge Misinzo.

Alisema alichukua hatua hiyo kwa sababu walinzi wa soko ni waajiriwa wa halmashauri.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama analitambua suala hilo, Ofisa Biashara huyo, alidai alipata taarifa juzi, ndipo akakemea tabia ya kuzoea matatizo ya wananchi na kumwamuru yeye na wasaidizi wake, wachange hiyo fedha na wamlipe hapo hapo sh. 600,000 zake.

 Alipopewa fedha hiyo, Yona alimshukuru Waziri Mkuu kwa kumsaidia arejeshewe mtaji wake.

Previous Post

TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIKAKATI KABAMBE UJENZI WA VIWANDA

MIKAKATI KABAMBE UJENZI WA VIWANDA

2 days ago
KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

9 months ago

Popular News

  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAKONDA ASISITIZA KULINDWA KWA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?