• ePaper
Saturday, August 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WANANCHI  wametakiwa kuhakikisha wanapima mitungi ya gesi kabla ya kuinunua ili kujiridhisha kuwa wanapata kipimo cha gesi kinacholingana na fedha wanazolipa, huku wafanyabiashara wote wa gesi wakikumbushwa kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo (WMA).

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Singida, Willie Amosi, wakati wa Maonesho ya 49 ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesema matumizi ya gesi ya kupikia yameongezeka kwa kasi kufuatia jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Amesema jukumu la Wakala wa Vipimo ni kuhakikisha kila mtungi wa gesi unaouzwa kwa wananchi unakuwa na kipimo sahihi cha gesi kama kilivyoainishwa na mzalishaji, ili kumlinda mlaji dhidi ya hasara inayoweza kusababishwa na vipimo visivyo sahihi.

“Wananchi wana haki ya kujiridhisha kuwa gesi wanayonunua ina uzito sahihi. Ndiyo maana sheria inamtaka muuzaji wa mwisho kuwa na mizani iliyohakikiwa na WMA ili kila mnunuzi aweze kupima mtungi wake kabla ya kuuchukua,” amesema Amosi.

Ameeleza kuwa kila mtungi wa gesi hubeba taarifa zinazoonyesha uzito wa mtungi wenyewe pamoja na kipimo cha gesi kilichomo ndani, hivyo mnunuzi anapaswa kulinganisha taarifa hizo kwa kupima mtungi kwenye mizani iliyothibitishwa.

Amosi amesema WMA inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wazalishaji, wafungashaji na wauzaji wa gesi nchini ili kuhakikisha vipimo sahihi vinazingatiwa, huku akibainisha kuwa malalamiko kuhusu upungufu wa gesi katika mitungi ya matumizi ya majumbani yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kuimarika kwa usimamizi.

Hata hivyo, amewataka wananchi kutoridhika na kupokea mitungi bila kupimwa, akisema ushiriki wao katika kuhakiki uzito wa gesi ni njia muhimu ya kulinda haki zao kama walaji na kuchangia uwajibikaji kwa wafanyabiashara.

Aidha, amewatahadharisha wauzaji wa gesi ambao hawana mizani inayotakiwa kisheria kuhakikisha wanaipata haraka, akisisitiza kuwa ukaguzi wa WMA unaendelea nchini kote na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kukiuka sheria.

Ametoa wito kwa wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nane Nane kutembelea banda la Wakala wa Vipimo ili kupata elimu kuhusu haki zao katika ununuzi wa gesi na bidhaa nyingine zinazouzwa kwa kutumia vipimo, akisisitiza kuwa usahihi wa vipimo ni msingi wa biashara ya haki na ulinzi wa maslahi ya mlaji.

Previous Post

MPASUKO SIMBA

Next Post

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA ZA TANZANIA

Next Post
RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA ZA TANZANIA

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA ZA TANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI MKUU AZINDUA BOTI MBILI ZA DORIA NA UOKOZI

WAZIRI MKUU AZINDUA BOTI MBILI ZA DORIA NA UOKOZI

2 weeks ago
OKELLO AING’ARISHA YANGA

OKELLO AING’ARISHA YANGA

3 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?