• ePaper
Saturday, August 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MPASUKO SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 4, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
MPASUKO SIMBA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

JOTO limezidi kufukuta katika klabu ya Simba baada ya viongozi wake wa juu kutofautiana kuhusu kutangazwa Baraza jipya la Wadhamini la miamba hiyo ya soka nchini.

Simba kupitia Mwenyekiti wake, Murtaza Mangungu, juzi ilitangaza baraza jipya la wadhamini lililoundwa na wajumbe saba ambao ni Salim Abdallah ‘Try Again’, Dk. Bill Kiwia, Alhaj Ismail Mohamed, Amos Makalla, Adam Mgoi, Hamad Abdallah na Hassan Hasanoo.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye, Makalla alitangaza kutokubaliana na uteuzi huo akidai haukufuata katiba ya klabu ya Simba.

Baada ya Mangungu kutangaza baraza hilo, Simba kupitia mitandao ya kijamii, ilichapisha taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori, ambaye alidai kuwa kikao kilichotangaza baraza hilo siyo kikao rasmi cha Mkutano Maalumu wa klabu hiyo.

Magori kupitia taarifa hiyo, alidai kuwa maamuzi yote yaliyotangazwa katika kikao hicho ni batili na kinyume cha katiba ya Simba.

“Kwa mujibu wa Katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho 2026, ibara ya 23, Mkutano Maalumu utaandaliwa na Mwenyekiti wa klabu kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi,” ilieleza taarifa ya Magori.

Pia, Magori   aliweka wazi kuwa, jana kulitarajiwa kuwa na kikao cha Bodi ya klabu hiyo kujadili ajenda ya Mkutano Mkuu Maalumu wa wanachama wa miamba hiyo.

Kufuatia kauli ya Magori, jana Mangungu  aliweka wazi  kuwa, alitangaza baraza hilo jipya baada ya kushauriana na Rais wa Simba, Mohamed Dewji.

“Mohamed ndiye aliyempendekeza, kuhusu kumshauri au hakumshauri hilo sio jukumu langu ,lakini hata hivyo anayo haki ya kukubali au kukataa kwa sababu bado hajapewa barua ya uteuzi,”

Mangungu alikiambia kituo kimoja cha redio, jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa, Mo alichangia majina manne na majina mengine matatu yametoka upande wa wanachama ambao unaongozwa na Mangungu.

SIMBA INAONGOZWA NA BODI-MAGORI

Akizungumza kwa njia ya simu na kituo cha redio,  Magori alisisitiza kuwa, Simba inaongozwa na bodi na siyo kitu kingine.

 “Hayo majina yametolewa kwa uhalali wa nani? au kwenye bodi ipi?, anajua kikao kinafanyika Jumatatu saa 9 mchana (jana) juu ya jambo hilo,” alisema.

Aliongeza kuwa, ameshangaa baada ya baraza jipya kutokuwa na Athuman Kapuya na Ramesh Patel.

“Hili jambo halivumiliki hata kidogo, katika hili, tutalifanyia kazi na tunajua wapo watu wanawatumia hawa.

“Watuoneshe katiba inavyosema, hili la ajenda hizo linajadiliwa Jumatatu (jana), kikao kimeitishwa tangu Ijumaa, leo unakuja kuondoa watu bila ya idhini ya bodi, hili halivumiliki,”alisisitiza Magori.

UHURU ilipomtafuta Mo Dewji kuthibitisha kama anaungana na Mangungu au Magori, simu yake iliita bila majibu.

Previous Post

DK. MWIGULU : TUBORESHE VIWANGO KWENYE BIDHAA

Next Post

WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU

Next Post
WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU

WAKALA WA VIPIMO WAELEZA TIBA YA GESI PUNGUFU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU APIGILIA MSUMARI

MWIGULU APIGILIA MSUMARI

7 months ago
MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

3 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?