Na REHEMA MAIGALA
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Chama kinaheshimu maoni ya wanasiasa na vyama vyote vya upinzani.
MAWAZO MBADALA
Pia, CCM imesisitiza iko tayari kuyafanyia kazi mawazo yenye msingi kutoka kwa vyama vya upinzani kwa maslahi mapana ya nchi.
Kihongosi alisema hayo jijini Dar es Salaam, katika kipindi kinachorushwa hewani na Redio Clouds, ambako alizungumzia masuala mbalimbali na hali ya siasa nchini.
Alifafanua, wanasiasa wanapaswa kutumia nafasi walizonazo kutoa ushauri unaolenga kuisaidia serikali na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Kihongosi alisema vyama vya upinzani vinapaswa kutoa ushauri kwa serikali kuhusu masuala yanayopaswa kufanyika, badala ya kulalamika bila kueleza sababu na nini kifanyike.
“Kiongozi mzuri ni yule anayelalamikia jambo na wakati huo huo kueleza namna ambavyo changamoto hiyo inaweza kutatuliwa,”alisema Kihongosi.
HALI YA SIASA
Akizungumzia hali ya kisiasa, Kihongosi alisema hali ya siasa nchini kwa sasa ni shwari, hivyo wanasiasa wanapaswa kutumia vyema nafasi hiyo kujenga siasa zenye maelewano mazuri.
“Ni vyema Tanzania kuwa na siasa zinazolenga kuleta maelewano ndani ya nchi, hizo ndizo siasa safi ndani ya taifa,” alisema Kihongosi.
MATUKIO YA OKTOBA 29
Kuhusu matukio ya Oktoba 29, mwaka jana, Kihongosi alisema wanasiasa hawapaswi kuyatumia kama mtaji wa kujijenga kisiasa, kwa kuwa walioathirika ni wananchi na watoto wa kawaida.
“Hakuna mtoto wa mwanasiasa aliyeathirika katika matukio ya Oktoba 29, hivyo wanasiasa tusitumie matukio yale kwa Chama hicho, Tundu Lissu,”aliongeza.
Katika hatua nyingine, Kiongosi alitoa wito kwa wanasiasa kudumisha upendo, amani na mshikamano akisema siasa zinapaswa kuwa sehemu ya kujenga nchi na si kuigawa.




