• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI HOMERA ATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA WA FUTI ZA UJAZO BILIONI 223

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI HOMERA ATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA WA FUTI ZA UJAZO BILIONI 223
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati  Dk. Juma Homera ametangaza rasmi ugunduzi mpya wa Gesi Asilia yenye futi za ujazo  Billion 223 katika kisima cha Kasa kilichopo Katika Kitalu cha Mnazi Bay Mkoa  Mtwara.

Dk. Homera amefanya uzinduzi huo tarehe 27 Oktoba,  2026 na kusema kuwa hilo ni tukio kubwa katika maendeleo ya sekta ndogo ya mafuta na gesi nchini na  kutoa shukrani za shati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono, miongozo na jitihada zake za kuhakikisha nchi inaendelea kupiga hatua katika Sekta ya Nishati.

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo gesi asilia iliyogunduliwa mwaka 1974, baadaye kuendelezwa na kuanza uzalishaji wake mwaka 2004, chango wa gesi asilia umekuwa mkubwa katika kuzalisha umeme na kutumika kama nishati viwandani, majumbani na kwenye magari.

Serikali imefanikisha haya kupitia Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na wawekezaji binafsi wa Makampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi (IOCs).

Ugunduzi huo umeshuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta, Dk. Jamese Mataragio, Menejimenti ya Wizara ya Nishati, Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

” Ni ukweli usiopingika kwamba kasi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali nchini, ikiwemo viwanda, ni kubwa. Hali hii inachochea ongezeko kubwa la mahitaji ya nishati kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi mengine viwandani na majumbani. Matarajio ya Watanzania yamebadilika, na kwa kiasi kikubwa wanahitaji nishati safi, salama, himilivu na ya uhakika”, alisema Dkt. Homera.

Serikali  imejipanga kuhakikisha miradi yote, ikiwemo ya nishati, inatekelezwa  ndiyo maana, TPDC na mbia wake kwa mara Kwanza baada ya Miaka 10 wamefanya utafiti na kugundua gesi asilia Katika kisima cha Kasa tangu mara ya mwisho ilipogundua gesi nchini mwaka 2015.

Amefafanua kuwa TPDC ilikuwa mbia katika Kitalu cha uzalishaji wa gesi asilia cha Mnazi Bay kwa asilimia 20, na iliongeza ushiriki wake kwa kununua hisa hadi kufikia asilimia 40 mwaka 2024, hatua iliyongeza ushawishi wa TPDC katika maamuzi ya kimkakati ya uendelezaji wa Gesi katika Kitalu hicho.

Upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha na ya uhakika unatarajiwa kupunguza gharama za nishati kwa viwanda na kaya, kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuchochea ukuaji wa viwanda.

 Vilevile, gesi asilia inaweza kutumika kama malighafi ya bidhaa za petrokemikali zikiwemo plastiki na mbolea, hivyo kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza thamani ya rasilimali za ndani.

Mradi huo utaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, unaimarisha usalama wa nishati nchini na kupunguza utegemezi wa nishati inayoagizwa kutoka nje, ambayo bei na upatikanaji wake huathiriwa na mabadiliko ya soko la kimataifa na migogoro ya kisiasa.

 Amefafanua kuwa baada ya Ugunduzi huo, TPDC imeingia katika majadiliano na wawekezaji wanne (4) wanaopanga kuendeleza miradi midogo ya gesi asilia kimiminika (LNG), ambapo watatu (3) wanatarajiwa kutekeleza miradi yao Mtwara. Miradi hiyo itaongeza ajira na kuchochea matumizi ya gesi asilia kwenye magari kama mbadala wa petroli na dizeli.

 Zaidi ya asilimia 80 ya gesi asilia inayozalishwa katika Kitalu cha Mnazi Bay hutumika kuzalisha umeme kupitia mitambo ya TANESCO iliyopo Mtwara na Dar es Salaam.

Aidha amezipongeza Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati, Menejimenti ya Wizara, Bodi za Wakurugenzi wa Taasisi zikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Wakuu wa Taasisi wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, pamoja na Timu ya Wataalam kwa ushirikiano walioutoa hadi kufanikisha Kazi hiyo.

Pia, amesema ongezeko la uzalishaji wa gesi asilia linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kupitia mgawo wa Gesi ya Faida (Profit Gas) kwa mujibu wa Mkataba wa Ugawanaji wa Mapato ya Petroli (PSA), mapato ya TPDC kama mbia, na kodi mbalimbali pia shughuli za kiuchumi zinazohusiana na mradi zitachangia kuongeza mapato ya Halmashauri za Mkoa wa Mtwara.

Takribani Watanzania 200 wameajiriwa katika shughuli mbalimbali kupitia kampuni za kizawa, na zabuni 35 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 20 zimetolewa kwa wazawa.

Katika shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi, asilimia 95 ya waajiriwa ni Watanzania, huku Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba kikiendeshwa kwa asilimia 100 na Watanzania.

 Amesema Mafanikio hayo yanaimarisha ushiriki wa wazawa, uhamishaji wa ujuzi na uwezo wa kitaifa katika sekta ya mafuta na gesi.

Previous Post

SANGU : MICHANGO YA WANACHAMA PSSSF INALINDWA, INAKUA NA KUREJESHA FAIDA

Next Post

WATAALAMU JIPANGENI TUPATE TRILIONI 7.3/ COP 31- MUYUNGI

Next Post
WATAALAMU JIPANGENI TUPATE TRILIONI 7.3/ COP 31- MUYUNGI

WATAALAMU JIPANGENI TUPATE TRILIONI 7.3/ COP 31- MUYUNGI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MGOMBEA URAIS AAHIDI UTEKELEZAJI BARABARA KIBAHA – CHALINZE – MORO

MGOMBEA URAIS AAHIDI UTEKELEZAJI BARABARA KIBAHA – CHALINZE – MORO

1 year ago
IBENGE ALIA NA WASHAMBULIAJI

IBENGE ALIA NA WASHAMBULIAJI

11 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?