• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WANANCHI MAGU WAELEZA KWA UFASAHA AHADI ZA DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 30, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
MGOMBEA Mwenza wa Urais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Magu
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Magu

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wilayani Magu, mkoani Mwanza, wamemdhihirishia Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kwamba wameelewa vizuri ahadi za siku 100 zilitolewa na Mgombea Urais CCM Dk. Samia Suluhu Hassan, iwapo atapewa ridhaa kuunda serikali.

Hayo yamejidhihirisha baada ya mamia ya wananchi na wanaCCM kujitokeza kumlaki Dk. Nchimbi wilayani humo na kuelezea kwa ufasaha ahadi hizo zilizotolewa na Dk. Samia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, jijini Dar es Salaam.

Awali, Balozi Dk. Nchimbi aliwaomba wakazi hao waeleze walivyomsikiliza Mgombea Urais wa Chama, Dk. Samia  kuhusu kazi atakazozifanya siku 100 za kwanza atakapopewa ridhaa ya kuiongoza nchi.

Alitaja miongoni mwa kazi atakazozifanya Rais Dk. Samia  ni ajira mpya kwa walimu 7,000 wa masomo ya sayansi na hesabu, kupiga marufuku kizuizi cha maiti hospitalini kwa sababu ya gharama, kuboreshwa kwa huduma za afya, bima ya afya kwa wote hususan makundi maalumu na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza-Isaka.

Mengine ni ujenzi wa madarasa na kuongeza shule za msingi miongoni mwa ahadi zinazogusa maisha yao.

Baada ya maelezo ya wananchi hao, Balozi Dk. Nchimbi  aliwaambia wananchi hao ameridhishwa na namna walivyoelewa ahadi za Dk. Samia na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025/2030.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia, wilayani Magu, Dk. Nchimbi amesema Ilani imetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

Ameyataja mafanikio hayo ni kuongeka kwa vituo vya afya  kutoka vitano hadi saba, zahanati kutoka 34 hadi 43, huku vituo vya upasuaji magonjwa ya dharura vikiongezeka kutoka viwili hadi vitano.

Pia, shule za sekondari zimeongezeka kutoka 21 hadi 41 na madarasa kutoka 268 hadi 780, huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 53 hadi asilimia 63, huku vijiji vinavyopata maji vikiongezeka kutoka 44 hadi 73.

Amesema upatikanaji wa umeme umeongezeka kutoka vitongoji 121 hadi 136, miradi ya umwagiliaji imefikia 12, majosho 19, mabwawa 145 na vizimba vya samaki kutoka 32 hadi 109.

Katika sekta ya miundombinu, barabara za lami zimeongezeka na kufikia kilometa 175 hali ambayo imefanya Magu kuwa mfano wa maendeleo vijijini na mijini.

Balozi Dk. Nchimbi alisema  endapo yeye na Rais  Dk. Samia watapewa ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili, watahakikisha mafanikio yaliyopatikana kipindi cha miaka minne ya  Rais Dk  Samia yanaimarishwa na kuongezwa maradufu, hususan sekta za elimu, afya, miundombinu, maji na umeme vijijini.

Akiwa Kisesa, Balozi Dk. Nchimbi, alisema serikali imejenga kituo cha afya, kuongeza madarasa katika shule ya msingi, kujenga maabara na huduma ya maji kutoka asilimia 44 hadi asilimia 73.

ameongeza kuwa, wananchi 73 kati ya 100 wanapata majisafi na salama, huku shule za sekondari na msingi zikiboreshwa.

AZURU KABURI LA HAYATI NYERERE

Balozi Dk. Nchimbi amezuru kaburi la Hayati Mwalimu Julius Nyerere lililopo Butiama, mkoani Mara.

Dk. Nchimbi aliweka shada la maua katika kaburi hilo na kuwasha misumaa na kufanya ibada fupi na baadhi ya viongozi na wanafamilia wakiongozwa na mtoto wa Hayati Nyerere, Madaraka.

Previous Post

MAELFU WAZIDI KUMIMINIKA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA CCM DK. SAMIA

Next Post

BALOZI DK. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE

Next Post
MGOMBEA Mwenza wa Urais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Butiama, mkoani Mara. (Picha na Abdurahman Jumanne)

BALOZI DK. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

3 months ago
UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

2 days ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?