• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA AMETEKELEZA MIRADI MINGI YA MAENDELEO – DK. NCHIMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 31, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AMETEKELEZA MIRADI MINGI YA MAENDELEO – DK. NCHIMBI
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Mara

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa ya kutafuta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, Balozi Dk. Nchimbi amewashukuru viongozi wa CCM, mkoani Mara kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa kishindo.

Balozi Dk. Nchimbi ameyasema hayo wilayani Bunda, mkoani Mara, alipowahutubia wananchi wa Bunda, waliokuwa wamesimama njiani kuupokea msafara wake uliokuwa ukitokea wilayani Magu, mkoani Mwanza.

Mgombea huyo yupo mkoani humo katika kampeni za uchaguzi wa CCM za kunadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya mwaka 2025-2030 na kuomba ridhaa kwa wananchi kuwachagua Rais Dk. Samia, wabunge na madiwani wa Chama katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu, kwa kukiipa ushindi wa kishindo, wapate ridhaa ya kuiongoza nchi kipindi kingine cha miaka mitano.

Akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo, Balozi Dk. Nchimbi amesema Rais Dk. Samia amefanya kazi  kubwa ya kutafuta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo maeneo mbalimbali.

“Rais Dk. Samia na wasaidizi wake wamezisimamia fedha hizo kuhakikisha zinaleta maendeleo kwa wananchi,” amesema.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA BUNDA

Mgombea Mwenza wa Urais Dk. Nchimbi, ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana wilayani humo  kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia ni kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Chifu Manyori, bweni la watu wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Madaraka.

Pia, ujenzi wa Kukirango na mradi mkubwa wa maji wa Mugango–Kiabakari unaendelea.

WALICHODHAMIRIA MIAKA MITANO IJAYO

Balozi Dk. Nchimbi amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo iwapo watapata ridhaa ya kuongoza nchi wamedhamiria kujenga soko la wilaya na stendi ya Kiabakari.

ASISITIZA AHADI SIKU 100 ZA KWANZA

Mgombea huyo ameendelea kusisitiza ahadi za siku 100 zilizotolewa na Rais Dk. Samia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, jijini Dar es Salaamu.

Amezitaja baadhi ya ahadi hizo ni kukomesha utaratibu wa kuzuia maiti hospitalini kwa kigezo cha  gharama , Bima ya  afya kwa Wote hususan kwa wajawazito, wazee, watoto, watu wenye ulemavu na ajira kwa  watumishi 5,000  wa kada ya afya.

Previous Post

DK. NCHIMBI : CCM INAJIVUNIA MTAJI MKUBWA WA WANACHAMA

Next Post

DK. NCHIMBI AAHIDI FURSA KWA VIJANA

Next Post
DK. NCHIMBI AAHIDI FURSA KWA VIJANA

DK. NCHIMBI AAHIDI FURSA KWA VIJANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

1 month ago
DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.