• ePaper
Saturday, November 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

MAAGIZO YA DK. MWINYI KWA WATUMISHI Z’BAR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 26, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
MAAGIZO YA DK. MWINYI KWA WATUMISHI Z’BAR

DK. HUSSEIN MWINYI

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU,

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo na uwajibikaji wakizingatia misingi ya utumishi na utawala bora ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema lengo la serikali ni kuimarisha zaidi maslahi ya watumishi wa umma nchini, kulingana na ukuaji wa uchumi na kuwa serikali imedhamiria kufikia asilimia 10 kutoka ukuaji wa sasa wa asilimia 7.4.

Dk. Mwinyi, aliyasema hayo, alipozungumza na watumishi wa umma katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema kuwa, mageuzi na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika Sekta ya Utumishi wa Umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, yameonesha dhamira ya kweli ya serikali ya kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma bora na kwa wakati.

Alisema katika kipindi hicho, serikali imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha utumishi wa umma, ikiwemo kuboresha mazingira ya kazi, kuongeza mishahara, posho na pensheni kwa wastaafu.

Alisema serikali imejipanga kuimarisha mifumo ya kidijitali kwa dhamira ya kurahisisha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi na kupunguza urasimu katika taasisi za umma.

Pia, alisema Serikali imeanzisha mifumo mbalimbali ambayo tayari imeleta ufanisi mkubwa, ukiwemo Mfumo wa Taarifa za Watumishi na Malipo (HCMIS), ambao umeleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa rasilimali watu na malipo ya watumishi.

Hivyo, aliwataka watumishi hao kuwa tayari kuipokea na kuitumia mifumo hiyo ili kuongeza ufanisi.
Alibainisha kuwa, katika kipindi cha kwanza cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane, Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko na changamoto katika sekta ya utumishi.

Alieleza kuwa, Serikali imeweka mifumo inayozingatia kiwango cha elimu, uzoefu na muda wa ajira, hatua ambayo imechangia kuongeza ari ya watumishi katika kuwatumikia wananchi.

Alisema Serikali imewapatia mafunzo watumishi 1,519 waliopata fursa za mafunzo ya muda mrefu ndani ya nchi, watumishi 65 waliopata mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi, na wengine 631 waliopata mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi.

Alisema lengo la Serikali ni kuwa na kizazi kipya cha watumishi wenye maarifa, ujuzi na mitazamo mpya inayolenga kuimarisha utumishi na maendeleo ya taifa.

Naye, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, aliwataka watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla, kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, mwaka huu kupiga kura na kumchagua kiongozi mwenye maono ya kuendeleza maendeleo nchini.

Previous Post

DK. SAMIA AVUTIA MAELFU KILA KONA

Next Post

SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

Next Post
SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA  AKICHAGULIWA OKTOBA 29

DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA AKICHAGULIWA OKTOBA 29

2 months ago
DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

1 month ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE YA KWANZA KWA GAMONDI STARS LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MARIDHIANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.