• ePaper
Friday, April 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA VIONGOZI WA DINI NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 17, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA VIONGOZI WA DINI NCHINI

RAIS DK. SAMIA SULUHU HASSAN

0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAULI ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa maridhiano nchini imepata uungwaji mkono kutoka taasisi na viongozi wa dini, huku wachambuzi wa siasa wakisema ni hatua itakayokuwa nguzo ya kurejesha imani ya wananchi kwa serikali na hatimaye kujenga mustakabali mpya.

Katika siku za hivi karibuni, mijadala kuhusu maridhiano imechomoza kama lugha mpya ya matumaini, inayowapa wananchi taswira ya Taifa.

Hatua hiyo, inakuja baada ya kutokea vurugu siku ya uchaguzi Oktoba 29, mwaka huu zilizosababisha uharibifu wa mali za watu binafsi, miundombinu ya umma na maisha ya watu.

Kutokana na matukio hayo, akiwa bungeni jijini Dodoma, Rais Dk. Samia alitangaza kuhuzunishwa na vifo vilivyotokea, huku akitoa pole kwa wafiwa na waliopoteza mali.

Rais Dk. Samia aliambatanisha ujumbe wake huo na ahadi ya kutochoka kunyoosha mkono katika maridhiano, akiwasihi wadau wahakikishe wanapokea vyema dhamira yake hiyo.

“Kwa kuwa wananchi wa Tanzania wamenipa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi hii, sitachoka kunyoosha tena mkono wa maridhiano. Ni matumaini yangu kuwa wadau wa kisiasa wataupokea kwa dhati mkono wa maelewano, ili kwa pamoja tujenge mazingira mwafaka kwa maendeleo ya Taifa letu,” alisema.

Kauli ya KKKT

Katika tamko la Novemba 12, mwaka huu, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) liliishauri serikali kusikiliza na kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa namna itakayodumisha umoja wa kitaifa.

Kanisa hilo, lenye ushawishi mkubwa nchini, lilisema suluhu ya kweli haiwezi kujengwa juu ya ukimya au kutazamana kwa shaka, bali kwa kusikilizana na kukiri kuwa palitokea makosa yanayohitaji kushughulikiwa.

Wakati huo huo, Shura ya Maimamu nchini ilitoa tamko lililohimiza jitihada zozote za kujenga umoja wa kitaifa kwa kuzingatia ukweli na uadilifu, hasa matukio yaliyosababisha hofu na majeraha ya kijamii.

Wanachosema wachambuzi

Akizungumzia hilo, mchambuzi wa masuala ya siasa na utawala, Dk. Edward Makundi alisema kauli ya taasisi hizo za dini ni kielelezo cha jinsi jamii inavyohitaji sauti ya maadili katika kipindi hiki cha mpito.

“Tunaposema maridhiano, tunazungumzia suala linalogusa hisia na kumbukumbu za watu. Taasisi za dini zina nafasi kubwa kwani zinaaminika na zinagusana moja kwa moja na wananchi. Kwa hiyo, uungwaji mkono wao kwa kauli ya Rais Dk. Samia unatoa mwanga kuwa sasa Taifa lipo tayari kuanza safari mpya,” alisema.

Maoni kama hayo yalitolewa pia na mchambuzi wa masuala ya jamii, Profesa John Shayo aliyesema maridhiano ni kama upasuaji, kwa kuwa hugusa sehemu yenye maumivu ili kupona.

“Taasisi za dini zimekuwa zikisisitiza jambo moja kwamba maridhiano ya kweli hayawezi kumilikiwa na upande mmoja. Ni lazima yashirikishe kila mdau muhimu, iwe ni serikali, vyama vya upinzani, jamii ya kiraia, vijana au makundi yaliyowahi kuguswa,” alisema.

Profesa Shayo alisema kauli ya Rais Dk. Samia imefungua dirisha litakalobadilisha mtazamo wa Watanzania kuhusu siasa, hasa kwa vijana ambao katika miaka ya karibuni wameonekana kutokuwa na imani na mifumo iliyopo.

“Rais amechukua hatua ya kipekee. Kuamua kuhutubia na kuzungumzia maridhiano hadharani kunahitaji ujasiri wa kukubali kuna baadhi ya mambo hayakwenda sawa. Hii ni ishara ya uongozi unaotaka kujenga upya,” alisisitiza.

Mchambuzi mwingine wa masuala ya siasa, Dk. Rose Mshangama alisema kama kuna kipindi ambacho Tanzania inahitaji sauti ya maadili, ni sasa.

“Tumeona michafuko ya kijamii, tumeshuhudia makundi yakipanga maandamano au yakionyesha hasira mitandaoni. Hii inaonyesha kuwa kuna jamii imepotoka lazima waelimishwe. Kauli za dini zinatupa mwongozo kwamba lazima utokane na ukweli na uwajibikaji,” alisema Dk. Mshangama.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke alisema wameisikiliza  vizuri hotuba ya Rais Dk. Samia alipohutubia Bunge kwamba ameonesha ana dhamira ya kweli ya kuleta maridhiano nchini.

Sheikh Kabeke alisema wanamuunga mkono Rais Dk. Samia kwa sababu viongozi wa mkoa huo walikuwa mstari wa mbele kufunga na kuomba dua mara kwa mara kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.

Alisema hotuba  ya Rais Dk. Samia imejaa dhamira nzuri ya mafanikio katika uongozi wake wa miaka mitano ijayo.

“Sisi viongozi wa dini tunampongeza Rais Dk. Samia kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa, tuna imani kubwa  kuwa atalivusha vyema Taifa letu hasa katika masuala ya amani na maendeleo nchini,”alisema Sheikh Kabeke.

 “Najua kila familia ina kijana au vijana, hivyo ni vyema kujiwekea msingi mzuri wa kukaa nao pamoja na kuelimishana umuhimu wa amani na utulivu nchini,”alisema.

Sheikh Kabeke alisema nchi isiyokuwa na amani na utulivu hata maendeleo yake yanachelewa kwa sababu hakuna muda kwa wananchi kufanya shughuli za uzalishaji mali.

“Uzalishaji mali unahitaji utulivu wa amani, hivyo vijana kwa kuwa ndio ndio tegemezi nchini hakikisheni msishawishike kuingia katika makundi ya hovyo yenye kutaka kuharibu amani ya nchi,”alisema.

Kwa upande wake kiongozi wa Alshwari Sunnah, Amani Mahuba alisema kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wamekuwa mstari wa mbele kuliombea Taifa.

“Tumeliombea Taifa letu kwa muda mrefu hivyo tunawaomba Watanzania wenzetu kwa pamoja tuwe na utulivu ndani ya nchi yetu,”alisema.

Naye, kiongozi wa Shia Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Hashimu alisema amani na utulivu hujenga uhusiano mzuri kati ya mtu na mtu.

“Amani yetu italeta mafanikio makubwa katika kuleta maridhiano ndani ya nchi yetu na kuwa na kuendelea kuwa na taswira nzuri ndani ya nchi yetu,”alisema Hashim.

Novemba 14, mwaka huu akilihutubia Bunge, Rais Dk. Samia alitangaza msamaha kwa vijana watakaobainika kufuata mkumbo na kushiriki vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

Alimwagiza Mkurugenzi waMashitaka (DPP), kuwaachia vijana hao iwapo watathibitika kutenda makosa ya uhalifu kwa kufuata mkumbo.

Pia, alitangaza kuundwa Tume Maalumu ya kuchunguza vurugu hizo kubaini chanzo chake na kwamba matokeo ya tume hiyo, yatasaidia kufanyia kazi changamoto zitakazobainika na kuliunganisha taifa.

Aidha, alisisitiza Tanzania imejengwa kwa misingi ya haki, uhuru na mshikamano, hivyo nguvu yoyote ya kuharibu misingi hiyo, haitakubalika.

Katika hotuba yake aliyotumia saa moja na dakika 34 (sawa na dakika 94), aliyoitoa wakati akizindua Bunge la 13, bungeni jijini Dodoma, Rais Dk. Samia alisisitiza uadilifu, uwajibikaji na utawala wa sheria, kuhakikisha wananchi wananufaika kupitia rasilimali zilizopo, ukiwemo upatikanaji huduma na serikali yake, itakoleza moto dhidi ya vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Previous Post

YANGA, SIMBA KAZI KAZI

Next Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

Next Post
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

4 months ago
KUWEKEZA KWA WANAWAKE NI MANUFAA YA JAMII

KUWEKEZA KWA WANAWAKE NI MANUFAA YA JAMII

3 months ago

Popular News

  • KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • LAZARUS CHAKWERA AMALIZA ZIARA YA SIKIU 9 NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?