• ePaper
Wednesday, July 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila

0
SHARES
67
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI MAALUM

TANZANIA imepongezwa kwa hatua kubwa ilizochukua katika kuzuia na kupambana na rushwa, hususan katika kuimarisha mifumo ya uzuiaji rushwa na utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa (UNCAC).

Pongezi hizo zimetolewa jijini Doha, Qatar, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila, akiwasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Mkataba huo katika Mkutano Mkuu wa 11 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa.

Chalamila, ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 19 Desemba, 2025, alisema rushwa bado ni changamoto kubwa kwa mataifa mengi duniani kwa kudhoofisha utawala bora, kukwamisha ukuaji wa uchumi, kuongeza umaskini, kukiuka haki za binadamu na kudhoofisha taasisi za umma.

Ameeleza kuwa Tanzania imefanikiwa kuimarisha mifumo ya kuzuia rushwa kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mpango wa Utekelezaji (NACSAP IV), pamoja na kuboresha mifumo ya manunuzi ya umma kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023.

Aidha, nchi imeimarisha taratibu za urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia za uhalifu ikiwemo rushwa, kupitia Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sambamba na kuziimarisha taasisi simamizi zikiwemo TAKUKURU, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Chalamila ameongeza kuwa, baada ya kukamilika kwa Mzunguko wa Kwanza wa Mapitio ya utekelezaji wa UNCAC uliofanywa na nchi za Austria na Msumbiji, Tanzania ilibainika kufanya mageuzi makubwa katika kuimarisha mfumo wa kitaifa wa kudhibiti uhalifu, utekelezaji wa sheria na ushirikiano wa kimataifa.

Mkutano Mkuu wa 11 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa hufanyika kila baada ya miaka miwili, ukiwakutanisha wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa, watunga sera, viongozi wa kisiasa, asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Previous Post

AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI

Next Post

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

Next Post
RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NEEMA LUKUKI BANDARI KILWA

NEEMA LUKUKI BANDARI KILWA

7 months ago
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

8 months ago

Popular News

  • MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • 50 BORA ‘FORM SIX’ KUSOMA AI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2/- YAKAMATWA IKITOROSHWA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAKA UADILIFU, USHIRIKIANO NA MATOKEO KWA VIONGOZI WAPYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?