• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Habari, Kitaifa
0
AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, ametoa maagizo ya mgawo wa maji kuwa shirikishi kwa kuwahusisha viongozi wa mitaa, nyumba na wilaya kuhakikisha ratiba ya upatikanaji wa maji inatekelezwa kwa ufanisi.

Aweso alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, katika kikao kazi na Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) aliowaagiza katika kipindi hiki cha mpito wa upungufu wa huduma ya maji uliojitokeza, wahakikishe ratiba ya mgawo inafika maeneo yote na maji yawe yanatoka siku nzima.

Alisema ushirikishwaji huo ni muhimu kwa sababu viongozi wa ngazi za chini wanafahamu kwa undani hali halisi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yao.

Waziri Aweso alisema kupitia ushiriki wa viongozi hao, inakuwa rahisi kufuatilia utekelezaji wa ratiba na kubaini maeneo ambayo hayajapata huduma kama ilivyopangwa.

Alieleza ratiba ya mgawo wa maji inapaswa kuwa wazi, wananchi wafahamu siku na muda watakaopata huduma, hatua itakayowapa nafasi ya kujiandaa mapema badala ya maji kuja ghafla na kuondoka bila manufaa.

Akitoa mfano wa maeneo ya Ubungo, Kimara, Mwananyamala, Manzese hadi Kinondoni, Aweso alisisitiza endapo ratiba itaonesha uwazi huduma ya maji itapatikana siku fulani, lazima timu za mamlaka husika ziwepo kuhakikisha maji yanawafikia wananchi kama ilivyoelekezwa.

Alisema ratiba ya maji lazima iendane na utekelezaji halisi na kujenga imani kwa wananchi.

Aidha, alielekeza Jiji la Dar es Salaam na Pwani kugawana kanda za mgawo wa maji kupunguza mzigo wa kusambaza huduma katika maeneo mengi kwa wakati mmoja.

“Kwa kufanya hivyo, kanda husika zitapatiwa maji muda mrefu zaidi badala ya huduma ya muda mfupi isiyokidhi mahitaji ya wananchi,” alisema.

Alisisitiza kumpatia mwananchi maji kwa siku nzima kunamwezesha kuhifadhi maji kwa matumizi ya siku kadhaa.

Kwa mujibu wa Aweso, mgawo wa maji usio na ratiba ya uwazi na unaotokea dakika chache hauna tija, hivyo kuagiza kuendelea kuboresha ratiba za upatikanaji maji, wananchi waelewe maana halisi ya ratiba hizo.

Juzi, Waziri Aweso katika mkutano kati ya DAWASA na wahariri wa vyombo vya habari wa kuzungumzia hali ya upatikanaji wa maji mkoani Dar es Salaam, aliitaka DAWASA kugawa maji kwa usawa, uwazi na kutoa ratiba, muda kwa eneo litakopata maji wananchi wapate muda wa kujiandaa.

“Ni wazi kuna vitu vingine viko nje ya uwezo wetu ikiwemo kuchelewa kunyesha mvua za vuli, niwaombe wananchi tuendelee kuwa na mshikamano katika kipindi hiki cha mpito.

“Nasisitiza DAWASA hiki kilichopo au tunachozalisha gaweni maji hayo kwa usawa na uwazi kwa kueleza katika ratiba zenu ni saa ngapi maji yatatoka katika eneo linalokusudiwa huduma hiyo, wananchi wajiandaa kupokea maji, kwa kufanya hivyo itapunguza malalamiko,” alisema.

Aliongeza jambo hilo liwe shirikishi kwa watu wote ikiwemo wadau wa sekta binafsi watengeneze namna nzuri ya kugawa maji kwa kushirikiana na DAWASA katika visima vilivyochimbwa pamoja na kuielimisha jamii namna ya kutunza vyanzo vya maji na kulinda mazingira.

Previous Post

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

Next Post

TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA

Next Post
TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA

TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA  AHADI YA KONGANI

DK. NCHIMBI ATOA AHADI YA KONGANI

8 months ago
SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

3 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?