• ePaper
Saturday, May 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SERIKALI MATUMAINI KIBAO AFCON

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 17, 2025
in Burudani, Michezo
0
SERIKALI MATUMAINI KIBAO AFCON
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema ina matumaini makubwa, kikosi cha timu ya Taifa Stars kitafanya vizuri katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa, serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha timu inafanya vizuri zaidi msimu huu.

Msigwa alisema kuwa timu inaendelea na mazoezi nchini Misri ambapo kesho itatua Morocco tayari kwa michuano hiyo.

Alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri zaidi msimu huu na kuweka rekodi ya aina yake.

“Tuna matumaini ya kuvunja rekodi na kuvuka hatua ya makundi kutokana na maandalizi tuliyoyafanya kwa kushirikiana na TFF.

“Timu ipo vizuri chini ya Kocha Miguel Gamond ambapo hivi sasa inafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Morocco tayari kwa mashindano na tumetoa kila kitu kuhakikisha wachezaji wanakuwa na morali ya kutosha,” alisema Msigwa.

Alisema wamewaalika wadau mbalimbali kwenda Morocco kuhakikisha wanakwenda kujifunza fursa mbalimbali watakazozitumia msimu ujao ambapo Tanzania itakuwa moja ya nchi mwenyeji.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha alisema Watanzania wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuipa sapoti timu hiyo iweze kufanya vyema katika michuano hiyo msimu huu.

Alisema mbali ya Watanzania kwenda kuishangalia Taifa Stars, lakini watapata kujifunza fursa mbalimbali ambazo watazitumia katika msimu ujao wa michuano hiyo.

Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani nchini Morocco.

Katika michuano hiyo, Taifa Stars imepangwa kundi C na timu za Nigeria, Tunisia na Uganda.

Taifa Stars inatarajia kutupa karata yake ya kwanza Desemba 23, mwaka huu dhidi ya Nigeria, Desemba 27 dhidi ya Uganda kabla ya kumalizikana na Desemba 30, mwaka huu.

Previous Post

MWAKINYO APEWA MBINU YA KUMCHAPA MNIGERIA

Next Post

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC

Next Post
NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

5 months ago
UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

3 weeks ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?