• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PM MWIGULU ASISITIZA USHIRIKIANO VIONGOZI WA DINI, SERIKALI 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 26, 2025
in Habari, Kitaifa
0
PM MWIGULU ASISITIZA USHIRIKIANO VIONGOZI WA DINI, SERIKALI 

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na serikali katika kutoa elimu ya umoja, amani, kupinga chuki, migawanyiko na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mshikamano wa Taifa.

Amesema vita yoyote inayohusisha wenyewe kwa wenyewe huwa haina mshindi bali inawapoteza wote, huku akisisitiza mgawanyiko ndani ya taifa hauna mshindi bali una matokeo ya kushindwa wote kama Taifa.

Dk. Mwigulu alitoa wito huo aliposhiriki ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri la Azani Front jijini Dar es Salaam,

“Manufaa ya amani ni makubwa. Huleta maendeleo ya kiuchumi, huimarisha ustawi wa jamii na huwezesha kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa,” alisema.

Alisema serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake kulinda amani na usalama wa nchi, kuwajenga Watanzania na hususan vijana kuthamini dhana ya uzalendo kwa nchi.

“Tanzania imeendelea kuwa kielelezo cha umoja, amani, mshikamano na utulivu katika ukanda wetu na barani Afrika. Amani hii imejengwa juu ya misingi imara ya maadili, haki, kuheshimiana, uvumilivu na uzalendo,” alisisitiza.

Dk. Mwigulu alitoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za elimu na dini katika kuimarisha malezi ya watoto na vijana kwa kuwajengea misingi imara ya maadili.

Katika Ibada hiyo, Dk. Mwigulu aliungana na Rais Dk. Samia, kuwatakia Wakristo na Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Krismasi, huku akiwasishi kusherehekea kwa amani, upendo, utulivu, kudumisha mshikamano wa kitaifa kwa maslahi ya Taifa.

ASKOFU MALASUSA AKEMEA

Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu Dk. Alex Malasusa alikemea tabia za baadhi ya watu kuchafua taswira za watu wengine na kuichonganisha jamii.

“Kuna watu wakiona jamii imekaa pamoja kwa amani wao inawakosesha raha,”alieleza Askofu Malasusa.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATUMA UJUMBE WA AMANI

Next Post

SIMBACHAWENE ATAJA MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA

Next Post
SIMBACHAWENE ATAJA MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA

SIMBACHAWENE ATAJA MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

3 weeks ago
DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

2 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?