• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TAIFA STARS NA AFCON YA HESABU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 27, 2025
in Burudani, MAKALA BURUDANI, MAKALA MICHEZO, Michezo
0
TAIFA STARS NA AFCON YA HESABU
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA

ILE ndoto ya Watanzania kuishuhudia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikipata ushindi wake wa kwanza katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inaweza kukamilika leo wakati miamba hiyo itakapocheza mchezo wake wa pili wa kundi C dhidi ya Uganda.

Taifa Stars itachuana na Uganda saa 2:30 usiku katika mchezo wa kundi hilo utakaopigwa katika Uwanja wa Al Medina uliopo Rabat, Morocco.

Katika michuano hiyo ya nne kwa Tanzania kushiriki, miamba hiyo haijawahi kushinda hata mechi moja kati ya mechi 10 ilizocheza katika AFCON, ikitoka sare mara tatu na kufungwa mara saba.

Leo Tanzania itahitaji kuvunja mwiko huo kwa kupata ushindi wake wa kwanza katika AFCON dhidi ya Uganda maarufu The Cranes.

Katika kundi C linaloundwa na timu za Tanzania, Nigeria, Uganda na Tunisia, kikosi cha Gamondi ndicho pekee ambacho hakijawahi kuvuna pointi tatu wala kutinga hatua ya mtoano katika historia ya michuano hiyo, ambapo mara zote tatu zilizopita iliishia makundi huku wapinzani wake wakipata mafanikio mbalimbali.

Nigeria iliyokata tiketi ya kushiriki mara 21 imetwaa ubingwa mara tatu (1980, 1994 na 2013), Tunisia iliyoshiriki mara 22 imebeba ‘ndoo’ hiyo ya Afrika mwaka 2004 na Uganda iliyoshiriki mara nane ikimaliza nafasi ya pili mwaka 1978.

Wakati rekodi ya Tanzania kutofanya makubwa AFCON ikimweka mtegoni Muargentina Gamondi, makocha wa soka nchini wanaamini kama Taifa Stars itafanya mambo sahihi kwa wakati sahihi basi hakuna kitakachoshindikana.

Katika AFCON mwaka huu, Tanzania ilianza kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Nigeria wakati Uganda ikifungwa mabao 3-1 ilipocheza na Tunisia.

Ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano, Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo huo wa dabi ya Afrika Mashariki.

MAKOCHA HAWA HAPA

Kocha wa Mbeya City ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Mecky Mexime alisema kitu kikubwa ambacho Stars inapaswa kujiandaa vyema kimbinu kuhakikisha inashinda katika mechi zake.

“Katika mpira lolote linatokea hata kama timu hapo zamani ilikuwa na historia nzuri inaweza kufungwa muhimu ni namna ya kujipanga kuhakikisha unapata ushindi katika kila mchezo,” alisema.

Aliyekuwa kocha wa Yanga na Ruvu Shooting, Charles Mkwasa, alisema usikivu wa wachezaji juu ya mbinu za benchi la ufundi ni miongoni mwa sababu ya msingi inayoweza kuibeba Stars katika fainali za AFCON mwaka huu.

“Wachezaji wa Stars wafuate yale wanayoambiwa na benchi la ufundi, ninaamini wakishirikiana vyema watafanikiwa,” alisema.

Salvatory Edward ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Pamba Jiji, alisema umakini, kujitoa na usikivu mzuri wa mbinu za benchi la ufundi itakuwa silaha bora kwa Taifa Stars katika fainali hizo.

“Stars inapaswa kuzingatia umakini, kujitoa na kusikiliza maelekezo ya walimu, wakifuata hayo na wakishirikiana vyema basi watapata mafanikio makubwa na kufika mbali katika mashindano ya AFCON,” alisema Edward.

AFCON ZILIZOPITA

Katika fainali zote tatu zilizopita ambazo Stars ilishiriki, timu hiyo haijawahi kutinga hatua ya mtoano hata mara moja.

Katika michuano ya mwaka 1980 iliyofanyika Nigeria, Taifa Stars ilipangwa kundi A na timu za Nigeria, Misri na Ivory Coast.

Taifa Stars iliburuta mkia kwa pointi moja baada ya kutoka sare na Ivory Coast. Awali, ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Nigeria na mabao 2-1 ilipovaana na Misri.

Katika AFCON mwaka 2019 zilizofanyika nchini Misri, Tanzania ilipangwa kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya.

Taifa Stars ilimaliza katika kundi hilo ikiwa nafasi ya nne baada ya kufungwa mechi zote tatu.

Kikosi hicho kilichokuwa kikinolewa na Amunike, kilianza kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Senegal, kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kenya na kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.

Pia, Taifa Stars iliburuta mkia katika hatua ya makundi ya AFCON mwaka 2023 zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Ikiwa imepangwa kundi F, Stars ilivuna pointi mbili (nyingi zaidi ya AFCON ilizoshiriki awali), ikianza kwa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Morocco, sare ya bao 1-1 kutoka kwa Zambia na suluhu dhidi ya DRC.

TANZANIA ILIVYOFUZU

Taifa Stars ilifuzu fainali hizo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa mwisho wa kundi H, kuwania kufuzu AFCON uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Bao la mshambuliaji nyota, Simon Msuva katika dakika ya 61, limeipeleka Tanzania katika AFCON baada ya kufikisha pointi 10 na kukwea hadi nafasi ya pili katika kundi hilo.

Msuva aliiandikia Stars bao katika dakika ya 61, akiuweka mpira kimiani kwa kichwa baada ya kuunganisha pasi ya Mudathir Yahya.

Bao hilo liliibua shangwe la aina yake kutoka kwa wachezaji na mashabiki walioujaza uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000.

SAFARI YA MABILIONI

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), michuano ya AFCON inatarajiwa kutumia dau la dola za Marekani milioni 32 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 78.3 za Tanzania kwa ajili ya zawadi pekee.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kuvuna dola za Marekani milioni saba ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 17.1.

Timu itakayoshika nafasi ya pili itavuna dola za Marekani milioni nne ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 9.7 za Tanzania.

Timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali, kila moja itaondoka na dola za Marekani milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 6.1 za Tanzania.

Timu nne zitakazoishia hatua ya robo fainali zitavuna dola za Marekani milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 3.1 za Tanzania.

CAF pia imeeleza kwamba, miamba minane itakayoishia hatua ya 16 bora itavuna dola za Marekani 800,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.9 za Tanzania.

Timu zitakazoishia nafasi ya tatu katika kundi, kila moja itaondoka na dola za Marekani 700,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.7 wakati zile zitakazoburuta mkia katika kila kundi zitavuna dola za Marekani 500,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.2 za Tanzania.

Previous Post

TANZANIA, UGANDA KATIKA TAKWIMU

Next Post

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

Next Post
DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ASISITIZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

RAIS DK. SAMIA ASISITIZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

2 weeks ago
RC MAKALLA  AKAGUA UJENZI UWANJA WA  AFCON ARUSHA

RC MAKALLA AKAGUA UJENZI UWANJA WA AFCON ARUSHA

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?