• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam

NA EMMANUEL MOHAMED

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yussuph Mwenda, amewaonya baadhi ya wamiliki wa bandari kavu (ICDs) wanaokwepa kodi ambapo amesisitiza hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika.

Kauli hiyo aliitoa jana katika kikao kazi kati ya Kamishna Mkuu wa TRA na wamiliki wa bandari hizo kilichofanyika jijini Dar es Saalam.

Alisema baadhi ya ICDs zinachochea kuweka mazingira ya ukwepaji wa kodi, hivyo TRA itaendelea kuzichukulia hatua kali.

“Najua kuna ukwepaji kodi unaofanyika katika baadhi ya bandari hizo za nchi kavu, tuna ushahidi lakini niliwaambia kuwa tunaziwezesha bandari zote kavu ziweze kufanya kazi kwa ufanisi. Mtaanza kusema sisi hatuhusiki. Watumishi wetu wapo pale, ninajua kinachoendelea ,”alisema.  

Kamishna huyo alisema kuna haja kuhakikisha TRA na wamiliki wa bandari hizo kushirikiana kufanya ICDs zinakuwa salama kwa maslahi ya umma.

“Kuna baadhi ya watu wanachagua ICDs kwa kudai kuwa wanazipenda kwa sababu fulani lakini hawazichagui kwasababu ya ufanisi bali kwa sababu zingine,”alisema.

Kamishna huyo aliwataka wamiliki wa bandari hizo kufanya kazi ya utoaji huduma ndani ya saa 24 ili kuongeza ufanisi katika eneo la usafirishaji wa mizigo.

“Katika kuhakikisha tunalifanyia kazi hilo, tutaleta rasilimali watu kutoka TRA hivyo lazima tuweke miundombinu ya kisasa ambayo itawezesha ufanyaji wa kazi wa saa 24,”alisema.

Alisema TRA itaendelea kuwapatia ushirikianao wamiliki wa bandari kavu ili wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Mwenda aliwaahidi wamiliki wa bandari hizo kuzifanyia kazi changamoto ambazo wameziwasilisha ikiwemo eneo la mifumo na utoaji wa leseni ya uendeshaji wa bandari kavu.

Naye, Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Juma Bakari, alisema uwepo wa bandari kavu zimetoa mchango mkubwa katika ukusanyaji mapato.

“Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, Idara ya Forodha ilikuwa inajukumu la kukusanya sh. trilioni 6.8. Kwa muda wa miezi sita tumefanikiwa kukusanya sh. trilioni 6.9 na tumezidia kwa asilimai 101.2,”alisema.

Alisema kitengo cha huduma cha forodha, kilikusanya sh. trilioni 3.6 ikiwa na lengo la kukusanya sh. trilioni 3.55.

“Ukichukua lengo la forodha la sh. trilioni 6.8 ambalo kitengo kilikusanya sh. trilioni 3.5 maana yake asilimia 52 ya makusanyo kwa kipindi hicho cha miezi sita, kimechangiwa na wadau wa ICDs waliopo hapa,”alisema. Mwenyekiti wa Wamiliki wa Bandari Kavu (CIDAT) Meleckzedeck Shange, alisema wadau hao wanakumbwa na baadhi ya changamoto ikiwemo upakiaji mizigo.

Previous Post

PM MWIGULU ASHUSHA RUNGU WIZARA YA MAJI

Next Post

MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA

Next Post
MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA

MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBASC KUWEKA HESHIMA CAFCL

SIMBASC KUWEKA HESHIMA CAFCL

2 months ago
NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?