• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PM MWIGULU ASHUSHA RUNGU WIZARA YA MAJI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PM MWIGULU ASHUSHA RUNGU WIZARA YA MAJI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Fred Alfred

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba ameipa Wizara ya Maji siku  14  kuhakikisha inakamilisha mchakato wa upatikanaji wa Mkandarasi wa ujenzi wa maji kutoka chanzo cha ziwa Chala.

Dk. Mwigulu aliyasema hayo katika muendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Amesema ujenzi wa mradi huo unapaswa kuanza kutekelezwa kwani unategemewa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Wilaya nzima ya Rombo.

“Natoa wiki mbili kwa wizara ya maji  kuhakikisha inakamilisha mchakato wa upatikanaji wa mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha Ziwa Chala.Mradi wa maji ziwa Chala unatarajiwa kugharimu kiasi cha sh.bilioni 8.6 na utanufaisha wananchi 34,104 katika vijiji 14 vya wilaya ya Rombo,”amesema.

ATAKA KUSIKILIZA WANANCHI

Katika hatua nyingine, Dk.Mwigulu aliwataka watumishi wa umma wanaopuuza kero za wananchi huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi yao.

Amesema ni muhimu watmishi kuacha kukaa ofisini bali wawafikiue wananchi na kutatua kero zao.

“Bado tunaendelea kupambana na wananchi wanaopuuza sauti za wananchi. Lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia ni kuona wanafanya kazi kwa uzalendo na uaminifu.

Ameongeza kuwa :”Tutaendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wazembe na wabadhilifu.

BARABARA

Kadhalika, Dk. Mwigulu amemuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha anatafuta fedha kwa ajili ya kufanya malipo ya awali kwa mkandarasi ili aanze ujenzi wa mradi wa barabara Holili (Rotima)-Tarakea(Nayemi) kilomita 52.8

Alisema Mradi huo ambao utagharimu kiasi cha sh. bilioni 28 unapita mpakani mwa Tanzania na Kenya na unategemewa kusaidia kukuza shughuli za kijamii, kiuchumi pamoja na utalii.

“Barabara hii ni muhimu kiuchumi na kibiashara kwasababu inaunganisha nchi mbili hivyo lazima tuhakikishe fedha zinapatikana kwa wakati kwa ajili ya kuanza ujenzi wake,”alisema

SHULE

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Stephen Moshi Technical ambayo itagharimu sh. bilioni 1.6  Dk. Mwigulu alisema kuwa shule hiyo ni kielelezo cha uwepo wa kiongozi mwenye maono na mipango.

“Ndani ya muda mchache sana zimejengwa shule zaidi ya 103 za aina hii nchi nzima” Alisema Dk. Mwigulu.

Aliongeza kuwa :“Rais Dk.Samia tangu ameingia madarakani amejenga shule 1300  na madarasa 79000 ili kiuhakikisha watoto wanapata elimu bila vikwazo.

Vilevile ndani ya siku 100 ameajiri walimu 7000 na kupelekwa katika vituo vya kazi kwa ajili ya kufundisha.

MIRADI YA KIMKAKATI

Dk. Mwigulu alisema Rais Dk.Samia ameendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati nchini.

Alisema miradi hiyo ni chachu ya  maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Hivi sasa ni Tanzania pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo ina umeme wa  ziada  zaidi ya megawati 2000 baada ya kukamilisha ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere.

Aliongeza kuwa :”Kazi yangu kama msimamizi wa serikali ni kuhakikisha maono ya Rais Dk. Samia yanatekelezwa kwa weledi na kikamilifu. Kila aliyepewa jukumu la kusimamia shughuli za serilaki atekeleze kwa umakini na weredi mkubwa.

AWESO

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema kuwa Wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa mradi huo na watahakikisha katika kipindi cha siku 14 wanampata mkandarasi wa mradi huo.

Alisema Rais Dk.Samia alipoingia madarakani aliahidi kumtua mama ndoo kichwani na kampeni hiyo ameitekeleza kikamilifu.

“Ndugu zangu niwahakikishie kuwa tutafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi mnapata maji ya kutosha ili kuendelea kutimiza adhma ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama bila vikwazo.

WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda alisema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwani imeenda sambamba na ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.Samia.

Alisema ziara hiyo iumeleta moshi mweupe katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara.

“Rombo tulikuwa na vituo vinne vya afya lakini hadi sasa vimefika nane hiyo ni hatua kubwa ambayo tunahitaji kumpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika wilaya zetu,”alisema Mkenda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rombo.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AFICHUA SIRI TANZANIA KUNG’ARA AU

Next Post

TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

Next Post
TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

3 months ago
WACHUMI WATAKA RAIS DK. SAMIA AUNGWE MKONO

WACHUMI WATAKA RAIS DK. SAMIA AUNGWE MKONO

3 days ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?