• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

AHMED ALLY ATULIZA MZUKA SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 27, 2026
in Burudani, Michezo
0
AHMED ALLY ATULIZA MZUKA SIMBA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally  amewatuliza mashabiki, wanachama wa klabu hiyo na kuwataka waache kutoa lawama kwa viongozi badala yake wawape sapoti.

Ally alisema hayo Dar es Salaam,jana, kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanachama wa timu hiyo wana shikamana na viongozi, timu ifanye vizuri katika mashindano yote yanayowakabili.

“Tumekuwa tunafanya vizuri misimu minane nyuma, kutokana na kuwepo umoja,  tumekuwa na historia hiyo kucheza robo fainali saba  za Bara la Afrika, kama itatokea tukashindwa basi mashabiki wanatakiwa kuacha kutoa lawama kwa viongozi na kuendelea kuisapoti.

“Hata kama tutachekwa na wapinzani wetu, lakini wanachama wa Simba wanatakiwa kutowalaumu viongozi wetu kwa sababu huu ni mpira,” alisema.

Meneja huyo aliongeza kwamba, viongozi hao ndiyo walisababisha timu yao ikafanya vizuri.

“Hao wanao tucheka, mwaka jana walishindwa kufanya vizuri katika mshindano ya msimu uliopita na kuishia njiani.

“Tuna uwezo wa kufanya vizuri katika michezo mitatu iliyobaki ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), “alisema.

Hata hivyo, Meneja huyo alisisitiza kwamba Simba ina nafasi ya kufanya vizuri katika michezo mitatu iliyobaki ya michuano (CAFCL).

Wiki iliyopita Simba ilipoteza mchezo wake wa tatu kwa kufungwa bao 1-0 na Esperance Tunis ya Tunisia.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza tena Januari 31, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Ally aliwaomba mashabiki, wanachama wa klabu hiyo kuwa kitu kimoja ana imani upepo huo mbaya utaondoka ndani ya klabu na kufanya vizuri kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori alisema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kutokata tamaa kwa vile Simba bado ina nafasi ya kufanya vizuri.

“Bado Simba ina nafasi ya kufanya vizuri katika michezo mitatu iliyobaki, hivi sasa mashabiki wasiiache timu bado nafasi ya kufanya vizuri ipo,” alisema Magori.

Previous Post

YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO

Next Post

‘BIRTHDAY’ YA MAZINGIRA

Next Post
‘BIRTHDAY’ YA MAZINGIRA

'BIRTHDAY’ YA MAZINGIRA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

4 weeks ago
AZAM FC YAIZAMISHA SIMBASC

AZAM FC YAIZAMISHA SIMBASC

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?