• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 27, 2026
in Burudani, Michezo
0
YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

UNAWEZA kusema kitaeleweka leo,Yanga na Dodoma Jiji zitakapo pambana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pambano hilo, limepangwa kupigwa katika Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Katika msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 19 baada ya kushuka dimbani mara saba.

Timu ya Dodoma Jiji ipo nafasi ya 11 katika msimamo wa michuano hiyo, ikiwa na  pointi 10 na imeshuka dimbani mara 10.

Akizungumza maandalizi ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Partick Mabedi  alisema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi ambao utawapa furaha mashabiki wa timu hiyo.

“Tunataka kurejesha nguvu yetu ya ushindi katika mchezo wa leo,pia maandalizi yako vizuri na wachezaji wana morali ya kutosha, wapo tayari kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema.

Mabedi alisema lengo lao katika mchezo wa leo ni kupata ushindi na kuirudisha heshima yao.

“Tunafahamu tutapata ushindani mkubwa kutoka wapinzani wetu nao wana wachezaji wengi wazuri,”alisema.

Mwakilishi wa wachezaji, Abubakari Ninju, alisema wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa leo, pia, kuwapa furaha mashabiki wa Yanga.

“Kwa niaba ya wachezaji tumejiandaa vizuri tupo fiti tutahakikisha tunacheza vizuri na kupata ushindi, tunatambua mchezo utakuwa mgumu, tumejiandaa kucheza katika kiwango kizuri ambacho kitatupa matokeo mazuri,” alisema.

Mchezaji huyo alisema wana amini watafanya vizuri mchezo wa leo kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki zao.

Kocha wa Dodoma Jiji,Amani Josia alisema jukumu kubwa kama walimu ni kuwaweka tayari wachezaji wao katika utayari wa kusaka ushindi dhidi ya Yanga.

“Lengo la mechi hii ni kuwapa furaha mashabiki zetu, ipo namna ya kupambana kuhakikisha tunapata ushindi katika mechi kama hizi kwasababu ya aina ya timu tunayoenda kukutana nao kuwa na wachezaji wengi wazuri wenye uzoefu mkubwa,” alisema.

Kocha huyo alisema wanaenda kukutana na Yanga, ambayo imetoka kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, Al Ahly.

“Yanga ina wachezaji wazuri hata kama wasipocheza waliocheza mechi na Al Ahly, bado wako vizuri tutacheza kutokana na kiwango chetu lengo ni kupata ushindi na kuondoka Dar es Salaam tukiwa na pointi tatu,” alisema.

Mwishoni mwa wiki, Yanga ilichapwa mabao 2-0 na Al Ahly katika pambano lililopigwa nchini Misri.

Timu hizo zinatarajiwa kupambana Januari 31,visiwani Zanzibar, ambapo maandalizi kuelekea pambano hilo yanaendelea kufanyika.

Previous Post

DK. MIGIRO AWATAKA MAWAZIRI KUHUDHURIA VIKAO VYA MASHINA

Next Post

AHMED ALLY ATULIZA MZUKA SIMBA

Next Post
AHMED ALLY ATULIZA MZUKA SIMBA

AHMED ALLY ATULIZA MZUKA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA

CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA

2 months ago
KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?