• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

DK. MIGIRO AWATAKA MAWAZIRI KUHUDHURIA VIKAO VYA MASHINA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 27, 2026
in Makala
0
DK. MIGIRO AWATAKA MAWAZIRI KUHUDHURIA VIKAO VYA MASHINA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na JOE NAKAJUMO

KATIKA bara la Afrika,Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka rekodi ya kuwa Chama kikongwe. Wiki ijayo, Februari 5, kitatimiza umri wa karibu nusu karne.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitakuwa kinasherehekea miaka 49 tangu kuundwa kwake Februari 5, mwaka 1977. Miaka hii siyo michache, kwani inafikia umri wa mtu mzima.

Kwa miaka yote hii, tangu kuundwa kwake, CCM, imemudu kuunda serikali katika pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.

UKOMAVU WA CCM

Swali linakuja, CCM, imewezaje kuwa imara miaka yote hii na muda wote kushika dola. Mshikamano na umoja miongoni mwa wanachama wake. CCM, imejiwekea msingi wa mizizi imara ya uongozi kuanzia ngazi ya chini na kuifanya iwe na ukomavu. Hili ni jibu la swali.

Ushahidi wa uwepo mshikamano na umoja, unaonekana wakati wa uchaguzi,uwe wa Chama au Serikali. Wagombea wa CCM wanapigana vikumbo wakati wa kampeni,matokeo yakishatangazwa na kumpata mshindi,wanarudi kwenye umoja wao. Aliyeshindwa anampongeza aliyeshinda bila kinyongo.

Baada ya uchaguzi,inatolewa ilani ya kuvunjwa makundi na wanachama kwa nidhamu wanarudi kuwa na mshikamano na umoja. Hivyo,kizazi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, kimelelewa, kuishi kwa misingi ya mshikamano, umoja na amani.  

 ZIARA DAR ES SALAAM

Mapema mwezi huu wa Januari, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Asha-Rose Migiro, alifanya ziara ya Chama, mkoani Dar es Salaam. Unaweza kuitaja kuwa ilikuwa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama. Alifanya mikutano na viongozi wa mashina ya Chama na mabalozi.

Katika mikutano na viongozi hawa wa ngazi ya chini, Katibu Mkuu, alieleza na kuhimiza umuhimu wa vikao vya  mashina, mabalozi na wanachama katika maeneo yao ikiwa moja ya hatua za kuimarisha Chama.

Dk. Migiro, aliwataka makatibu wa itikadi na uenezi,kushirikiana na viongozi wa mashina katika madarasa ya itikadi. Aliongeza kwamba mashina ndiyo darasa la kwanza la itikadi na wanachama watajifunza misingi ya CCM.

Sina hakika kama unaendelea utaratibu wa zamani wa mtu anayeomba kujiunga na CCM, anapaswa kwanza kuhudhuria masomo ya itikadi kwenye shina au tawi. Ni vizuri Katibu Mkuu, amekumbusha umuhimu wa madarasa ya itikadi.

UHAI WA CHAMA

Dk. Migoro anasema uhai wa Chama Cha Mapinduzi, unatokana na mashina na kwamba kupitia vikao, Chama kinaweza kujipima kina uwezo kiasi gani. Hivyo anasisitiza kufanyika kwa vikao na ni wajibu wa kila mwanachama, hasa viongozi kushiriki kikamilifu kwenye vikao.

Anafafanua kwamba ndani ya vikao kuna kubadilishana uzoefu na zitakuwepo taarifa sahihi za kukisukuma Chama Cha Mapinduzi ngazi zinazofuata.”

Mashina ndiyo darasa la kwanza la itikadi, kupitia mashina haya, kizazi kitajifunza historia ya Chama Cha Mapinduzi, historia ya nchi yetu na maana ya kuwa mwanaCCM,”anasisitiza Katibu Mkuu wa Chama.

MAAGIZO WABUNGE NA MAWAZIRI

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, ametoa maagizo kwa wabunge na mawaziri, kuhudhuria vikao vya ngazi ya mashina, kubaini changamoto zinazowakabili wananchi. Hatua hii, anasema ,itawawezesha wabunge na mawaziri kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali, zitakazoibuliwa katika vikao.

Anakumbusha kuwepo wabunge na mawaziri kwenye vikao vya mashina, kutawawezesha kubaini changamoto  walizoahidi kuzifanyia kazi katika Ilani ya Uchaguzi, baada ya kupokea dola. Anasema mabalozi wa mashina ni chemichemi ya fikra, macho, masikio na daraja linalounganisha Chama na wananchi.

“Viongozi wa ngazi za juu,tufanye vikao vya kikatiba kupata changamoto za wananchi na tushauri Chama ili kuishauri Serikali,”anasisitiza Katibu Mkuu  wa CCM.

TANU MWAKA 1966

Umuhimu wa mawaziri kuhudhuria vikao vya chini vya Chama,ulianza kusisitizwa tangu enzi za TANU. Oktoba, mwaka 1966, Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU, iliwataka mawaziri kufungua ofisi katika ofisi za Chama,ili shida za wananchi zisikike.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU katika mkutano wake wa siku moja,uliofanyika Dar es Salaam,Oktoba Mosi,mwaka 1966,iliagiza kwamba mawaziri wote wa serikali sasa itawabidi kuwa na ofisi zao katika Ofisi Kuu ya TANU ambako watakuwa  wakionana na wananchi kusikiliza shida zao.

AGIZO KWA MAWAZIRI

Halmashauri Kuu, iliwataka mawaziri wote,wakishirikiana na Ofisi Kuu ya TANU, wapange utaratibu na siku maalum, watakazokuwepo katika ofisi hizo mpya kungojea kusikiliza shida za wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya TANU, ilisema kuwa azimio hili pia linawahusu wakuu wa mikoa na wilaya ambao watafanya utaratibu maalumu wa kuwa na ofisi zao katika ofisi za TANU, watakaokuwa wanasikiliza shida za wananchi. Hawa watakuwa wanashirikiana na Mwenyekiti wa Chama katika kuonana na kusikiliza shida za wananchi.

Taarifa ya Makao Makuu ya Chama, imekumbusha kuwa  Serikali ni chombo cha wananchi cha kufanya na kutimiza kazi na kwamba TANU ndiyo watu wenyewe na kwa hivyo ofisi za TANU ndiyo mahali pa wananchi kuwasilisha shida na mashauri yao.

MAELEKEZO YA DK.SAMIA

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, mara kwa mara katika majukwaa mbalimbali amekuwa akiwahimiza viongozi kushuka chini kukutana na wananchi kujua kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwezi Agosti, mwaka jana 2025, katika hafla ya kuwaapisha viongozi,Ikulu Chamwino, Dodoma, Rais Dk.Samia, alitoa maagizo kwa wakuu wa mikoa nchini kusikiliza na kutatua kero za wananchi wanaowaongoza.

Dk. Samia alitoa maagizo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi kuzifahamu kero wanazokabiliwa nazo na kuzitafutia suluhu kwa kushirikiana na watendaji wengine.

KATIBU WA NEC

Novemba mwaka jana, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, alisema Chama Cha Mapinduzi, kitaisimamia serikali na hakitasita kuwachukulia hatua viongozi wavivu, wazembe na watakaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Alisema kile ambacho Watanzania waliahidiwa, lazima kitekelezwe, hivyo viongozi wanapaswa kuwajibika ipasavyo na wataweka vipimo vya uwajibikaji na utendaji kazi wa viongozi wa serikali kwa kuchekecha utendaji wao.

“Yule ambaye ufanisi wake utakuwa ni chini, Chama kitachukua hatua mara moja. Wale watakaofanya vizuri, Chama kitaendelea kuwalinda kuhakikisha kazi yenye matunda mema kwa Watanzania inafanikiwa,” alisisitiza Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo.

Kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, 2025—2030, kupitia ahadi za mgombea, Kihongosi aliwataka mawaziri na naibu mawaziri kutambua kuwa wajibu wa Chama ni kuisimamia serikali, siyo serikali kukisimamia Chama. Kazi imeanza,Chama kitaifuatilia serikali kuhakikisha yaliyoahidiwa katika kampeni yanatekelezwa.

BABA WA TAIFA

Oktoba mwaka 1976, Baba wa Taifa, Rais Mwalimu Julius Nyerere, alisema  serikali ni madaraka ya utawala na hutumia madaraka hayo kwa kupitia vyombo vilivyowekwa, wakati Chama  ni umoja wa wananchi waliojiunga kwa madhumuni maalumu na mara nyingi kwa shabaha ya kushika serikali ili itumiwe kutekeleza maslahi ya wananchi.

Mwalimu Nyerere alisema mara nyingi, serikali huogopwa kinyume na Chama ambacho lugha yake ni kueleza, kuelekeza na kuongoza kwa sababu Chama kinatokana na watu na ni cha watu wenyewe. (Mawasiliano na Mwandishi WhatsApp 0784291434;email nakajumoj@gmail.com)  

Previous Post

‘HAPPY BIRTHDAY’ RAIS DK. SAMIA, KINARA WA UTUNZAJI MAZINGIRA

Next Post

YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO

Next Post
YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO

YANGA, DODOMA JIJI KITAELEWEKA LEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

7 months ago
NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

6 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?