• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 27, 2025
in Habari, Kitaifa
0
DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima

0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, ametoa onyo kwa ‘watu wazima ovyo’ wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii, hususan kwa kuathiri usalama na maadili ya watoto.

Amesema serikali haitasita kuwafikisha mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, ya mwaka 2015 wanaofanya makosa hayo.

Dk. Gwajima alisema serikali imeona umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti kulinda watoto dhidi ya maudhui hatarishi na vitendo vinavyokiuka maadili na sheria

Alisema kuwa wizara yake imeunda kamati maalumu itakayojifunza uzoefu wa nchi nyingine zilizofanikiwa kudhibiti athari za mitandao kwa watoto, huku akieleza mapendekezo ya kamati hiyo yanatarajiwa kuwasilishwa ndani ya vipindi vijavyo vya Bunge.

MALENGO

Waziri Gwajima alisisitiza, hatua hizo hazilengi kuwanyima watu wazima uhuru wao wa matumizi ya mitandao, bali kulinda watoto ambao bado hawana uwezo wa kujilinda dhidi ya athari za maudhui yasiyofaa.

Akifafanua jukumu la wizara yake, Dk. Gwajima alisema Wizara ya Maendeleo ya Jamii imejipanga kikamilifu kwa kuwa na sera, miongozo na mifumo ya ulinzi inayofika hadi ngazi ya chini ya jamii. 

Alitaja uwepo wa Sera ya Wazee na Mabaraza ya Wazee, Miongozo ya Wajane, Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake na majukwaa ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na wafanyabiashara wadogo.

Kwa upande wa watoto, alisema kuna mabaraza ya watoto, madawati ya ulinzi wa mtoto katika shule za msingi na sekondari, vyuo vikuu na madawati ya jinsia katika masoko, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za watoto.

Dk. Gwajima aliwataka wananchi kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mikakati hiyo, akifananisha hali hiyo na maandalizi ya kilimo pale mawingu yanapoonekana, akisema hatua za mapema ndizo zitakazowezesha kulinda watoto na kuimarisha maendeleo ya jamii kwa ujumla.

VIONGOZI WA DINI

Mchungaji Dk. Joseph Isaya, alisema watu wazima wanaofanya hivyo wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwakuwa siyo kitu kizuri katika jamii hasa kwa watoto ambao wanaendelea kukua. 

Alisema picha hizo huwa zinaharibu watoto kisaikolojia, ndoa na hata kugombanisha wanafamilia kwa kuwa anayefanya hivyo huwa na maslahi yake lakini huwa inawaathiri watu wengi.

“Mtu anayefanya hivyo kiimani tunasema anaabudu sanamu, na hii haikubaliki kabisa, vijana wasitumie mitandao kupitiliza watumie katika kazi sio kwa namna mbaya,”alisema.

Alisema walimu, wazazi na walezi wanatakiwa kuongeza umakini katika malezi ya watoto, kwani mitandao ya kijamii huwa inatumika vibaya hivyo ni vizuri kufuata mila na desturi za nchi.

Kwa upande wake mchungaji wa Kanisa la EAGT Temeke, Joshua Isaack, aliikumbusha jamii kuwa miili ni uumbaji wa Mungu wenye thamani na heshima kubwa, hivyo haipasi kuitumia kama chombo cha kutafuta umaarufu au kuthibitishwa kupitia mitandao ya kijamii. 

Alisema picha za utupu zinapowekwa mitandaoni hupoteza heshima ya mtu binafsi na mara nyingi huacha majeraha ya muda mrefu ya kiroho, kisaikolojia na kijamii, hasa kwa vijana na watoto wanaoangalia na kuiga.

Mchungaji huyo alionya kuwa, uhuru bila mipaka hugeuka utumwa na akaisisitiza jamii kutumia hekima kabla ya kushiriki au kusambaza picha zisizo na staha

Alisema kanisa, familia na jamii wanao wajibu wa kushirikiana katika kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yanayoweza kuharibu mwelekeo wao wa maisha.

Aliwahimiza Watanzania kuchagua kile kinachojenga utu na kumpendeza Mungu, badala ya kile kinachoharibu heshima ya mwanadamu.

MWANASAIKOLOJIA/ OFISA USTAWI JAMII

Mwanasaikolojia kutoka OSHA, Rebecca Delem, aliieleza jamii kuwa kuweka picha za utupu mitandaoni mara nyingi huchochewa na hitaji la kuthibitishwa, kukubalika au kuonekana wa thamani kupitia maoni na alama za kupendwa. 

Alisema kuwa utegemezi huo wa uthibitisho wa mitandao unaweza kuathiri afya ya akili, kujenga hali ya kujidharau, msongo wa mawazo na kupoteza uhalisia wa thamani binafsi.

Rebecca alisema, picha zinazowekwa mitandaoni hubaki katika kumbukumbu za kidijitali kwa muda mrefu zinaweza kusambazwa nje ya udhibiti wa mhusika.

Alisema kwa mujibu wa taaluma ya saikolojia, hali hiyo huweza kusababisha majuto makubwa baadaye, aibu ya kijamii, unyanyapaa na hata changamoto za kisaikolojia pale mtu anaposhindwa kudhibiti athari za maamuzi aliyoyafanya awali.

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka Mkoa wa Mbeya, Magdalena Ngenzi, alisisitiza kuwa watoto na vijana wako hatarini zaidi, kwa sababu bado wako katika hatua ya kujitambua na kujijenga. 

Magdalena alisema kuona au kuiga picha za aina hiyo huweza kuvuruga maendeleo ya kisaikolojia ya mtoto, kupotosha uelewa wa heshima ya mwili na mahusiano, na kuongeza hatari ya kuathiriwa na shinikizo la rika.

Aliitaka jamii kujenga utamaduni wa kuwajibika kidijitali, kwa kufikiria madhara ya muda mrefu kabla ya kushiriki maudhui yoyote mitandaoni. 

Magdalena alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya wazi katika familia, shule na jamii kuhusu matumizi salama ya mitandao, akieleza afya ya akili na heshima ya mtu ni muhimu kuliko umaarufu wa muda mfupi.

Previous Post

TAIFA STARS NA AFCON YA HESABU

Next Post

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

Next Post
MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NDOTO YATIMIA

NDOTO YATIMIA

4 months ago
TANZANIA IPO SALAMA MIKONONI MWA CCM – PETER MSIGWA  

TANZANIA IPO SALAMA MIKONONI MWA CCM – PETER MSIGWA  

8 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?