• ePaper
Thursday, June 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 28, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na LATIFA GANZEL, Morogoro

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Rashid Paulo (35), mkulima na mkazi wa Msowelo kwa tuhuma za mauaji ya Steven Mayungu (26), mkulima na mkazi wa Mayungu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, alisema tukio hilo lilitokea, saa tano usiku katika Kitongoji cha Shuleni, Kata ya Lumuma, wilayani Kilosa.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alimchoma Mayungu na kitu chenye ncha kali eneo la kifuani, baada ya kutokea ugomvi kati yao unaodaiwa kusababishwa na wivu wa kimapenzi.

“Mtuhumiwa alimtuhumu Mayungu (marehemu) kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake,” alisema.

Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi huku utaratibu wa kisheria ukiendelea kufanyika.

Kamanda Mkama alitoa wito kwa wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi, badala yake watumie vyombo husika kutatua migogoro au matatizo ya kifamilia kwa njia ya amani na kufuata sheria.

Wakati huo huo, dereva Uwimpue Bonheur (33), raia wa Rwanda, mkazi wa Kigali alikamatwa akiwa anaendesha gari la mizigo lenye namba za usajili RAI 878 G aina ya HOWO akiwa katika hali ya ulevi kipimo 171.7mg/100ml akitokea Kigali kwenda Dar es Salaam.

Kamanda huyo alisema tukio hilo lilitokea jana asubuhi katika eneo la Kwachambo, Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Morogoro- Dodoma.

Alisema mtuhumiwa alizuiliwa kuendesha chombo hicho kwa usalama wake na wadau wengine wa barabara wakati hatua zingine za kisheria zikiendelea.

Mkama aliwataka madereva kutotumia ulevi wakiwa wanaendesha magari kuepusha matukio ya ajali zinazogharimu maisha ya watu, uharibifu wa miundombinu na mali.

Previous Post

 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

Next Post

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

Next Post
‘POLICE SERVICE’ GUMZO

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA  AKICHAGULIWA OKTOBA 29

DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA AKICHAGULIWA OKTOBA 29

9 months ago
MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

9 months ago

Popular News

  • WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?