• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 30, 2025
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

WAKATI wadau wa masumbwi wakitoa maoni tofauti kuhusu ushindi wa Mtanzania Hassan Mwakinyo na ubora wa mpinzani wake, Stanley Eribo, takwimu zinaonyesha Mnigeria huyo ni moto wa kuotea mbali na siyo ‘dhaifu’ kama inavyodaiwa.

Mwakinyo mwenye nyota tatu na nusu katika mtandao wa boxrec alimchapa Eribo mwenye nyota moja na nusu kwa TKO raundi ya pili katika pambano lisilo la ubingwa la raundi 10, uzito wa kati lililofanyika Ijumaa iliyopita katika  Ukumbi wa Warehouse, Dar es Salaam.

Katika mtanange huo uliohudhuriwa na mamia  ya mashabiki, Mwakinyo alimchakaza Eribo katika raundi ya pili baada ya kumpiga ngumi ya kidevu na Mnigeria huyo kusalimu amri.

Baada ya pambano hilo, wadau wa masumbwi walitoa maoni tofauti kuhusu pambano hilo huku wengine wakidai Mwakinyo alipigana na bondia dhaifu ambaye hakuwa na ushindani.

Akizungumza baada ya pambano hilo, bondia wa ngumi za kulipwa, Mtanzania Ibrahim Mgender maarufu Ibrah Class, alidai Mwakinyo alipigana na mpinzani asiye na uwezo mkubwa katika kurusha makonde.

“Mwakinyo anawaaminisha watu ni bora kwa kuleta mabondia wasiyo na uwezo wowote, yule bondia aliyecheza naye angecheza na mimi hata raundi ya kwanza asingemaliza, hata Mfaume Mfaume (bondia) angecheza naye nina imani angempiga mapema sana,” alisema Ibrahim Class.

Hata hivyo, baadhi ya wadau wametofautiana na maoni hayo ambapo wamesisitiza kuwa Eribo ni bondia mzuri ambaye alizidiwa na maarifa ya Mwakinyo.

Bondia wa zamani na aliyekuwa bingwa wa kick boxing, Japhet Kaseba alisema Mwakinyo alipata ushindi kutokana na ubora wake wa kuwapiga wapinzani maeneo ikiwemo kidevuni.

“Mapambano mengi ya Mwakinyo amekuwa akipata ushindi wa namna ile kwa kumpiga mpinzani eneo la kidevu, hakuna ngumi inayouma kama sehemu hiyo duniani kote, ndiyo maana Eribo alishindwa kuendelea kupigana.

“Mwakinyo ameona silaha yake kubwa ni kupiga eneo la kidevuni ndiyo maana amekuwa akifanyia mazoezi ya mara kwa mara, hivyo Watanzania wanapaswa kuelewa suala hili na kuachana na kumpa lawama ambazo hazina afya katika mchezo,” alisema.

Bondia wa ngumi za kulipwa, George Mbonabucha, alisema Mwakinyo alimzidi kiwango Eribo hatua ambayo ilimpa nafasi kubwa ya kushinda na siyo mpinzani kutokuwa na uwezo wa kupigana.

“Kuwa na nyota nyingi siyo tatizo, unaweza kuwa hauna nyota hata moja katika mtandao wa boxrec unawapiga mabondia mbalimbali, watanzania wanatakiwa kuelewa  Mwakinyo amejiandaa vizuri ndiyo maana amepata ushindi wa mapema,” alisema.

Mbonabucha alisema Watanzania wanapaswa kujivunia kuwa na mabondia wazuri akiwemo Mwakinyo ambao wanapata ushindi unaoleta heshima katika taifa na siyo kuwakatisha tamaa.

TAKWIMU HIZI HAPA

Wakati baadhi ya wadau wakitilia shaka uwezo wa Eribo, takwimu za mtandao wa boxrec zinaonyesha kuwa, Mnigeria huyo kabla ya kukutana na Mwakinyo, hakuwahi kupoteza katika mapambano 10 yaliyopita.

Katika mapambano hayo, Eribo alishinda mara tisa na kutoka sare mara moja hatua ambayo inamfanya bondia huyo kuwa na rekodi nzuri.

Eribo mwenye umri wa miaka 36, alitoka sare na  Prince Bakattah kutoka Ghana huku akiwapiga Saheed Lawal (Nigeria), Djamiou Ekpesso (Benin), Ramadhani Shauri (Tanzania), Isaac Sowah (Ghana), Dele Adeleke (Nigeria), Sunday Olalekan (Nigeria), Isiaka Malik (Nigeria), Saheed Olayiwola (Nigeria)na Yaw Sakiya (Ghana).

Previous Post

SIKU YA HISTORIA MPYA TAIFA STARS

Next Post

SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

Next Post
SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MPINA APIGWA ‘STOP’ URAIS ACT-WAZALENDO

MPINA APIGWA ‘STOP’ URAIS ACT-WAZALENDO

10 months ago
MWAKINYO APEWA MBINU YA KUMCHAPA MNIGERIA

MWAKINYO APEWA MBINU YA KUMCHAPA MNIGERIA

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?