• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 9, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema mradi wa umemejua unaotekelezwa wilayani kishapu mkoani Shinyanga utaleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya nishati na kiuchumi kutokana na kutoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa umeme wa uhakika utakaoingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Salome ameyasema hayo akiwa mkoani Shinyanga baada ya kutembelea mradi wa umemejua wa kishapu pamoja na ule wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli sambamba na njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli-Simiyu.

Amesema huu ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kupitia Mhe Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi inayotekelezwa na Serikali hususani ya umeme.

Kuhusu mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Mhe.Salome amesema umeme utakaozalishwa utawanufaisha wananchi wote wa Tanzania na kuleta mapinduzi kwani sekta ya umeme inawagusa mwananchi mmojammoja.

Akizungumzia maendeleo ya mradi huo, Meneja mradi wa Kishapu Mha.Emanuel Anderson amesema, mpaka sasa mradi umefikia zaidi ya asilimia 89 na unahusisha ujenzi wa paneli elfu 82 zenye uwezo wa Wati 605 kika moja zitakazozalisha megawati 50 za awali kwa awamu ya kwanza

Amesema mradi wa umemejua kishapu utakuwa wa manufaa makubwa kutokana na umuhimu wake kwenye utunzaji wa mazingira unaoepuka uzalishaji wa hewa ya ukaa na umeajiri Watanzania wengi kwa kipindi chote cha utekelezaji wake.

Akitoa tathmini ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme Kaimu Mkurugenzi wa Miradi ya umeme TANESCO makao Makuu Mha. Frank Mashalo amesema miradi hiyo inahusisha uongezaji na uwekaji wa Transfoma yenye uwezo wa MVA 780 ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na Mikoa jirani.

Aidha ameeleza kuwa miradi hiyo inatekelezwa na  Mkandarasi Sieyuan Electric kutoka China na Kalpataru kutoka India  anayetekeleza mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Shinyanga hadi Simiyu.

Awali kabla ya kuanza ziara yake Mhe Salome na ujumbe wake walipata fursa ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita ambaye alimshukuru Mhe.Salome kwa kazi nzuri anayoifanya kutembelea miradi inayotekelezwa na Wizara ya nishati chini ya taasisi zake.

Miradi yote ya upanuzi wa kituo cha kupoza umeme njia ya kusafirisha umeme kutoka Shinyanga hadi Simiyu na ule wa umemejua wa kishapu imegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

Previous Post

KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

Next Post

TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

Next Post
TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

2 weeks ago
RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

3 weeks ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?